Kama ambavyo maandalizi sahihi hufanyika katika shughuli yeyote ya kimaendeleo, katika kilimo hai pia kanuni ya haki na usawa pamoja na uangalizi visipozingatiwa vyema mkulima hawezi kufaidika na kilimo hai. Kanuni ya haki na usawa Kilimo hai sharti kizingatie msingi wa mahusiano yatakayohakikisha usawa katika mazingira na fursa ya kuishi.Usawa unaojali na kuzingatia heshima, haki na kujituma kwa kila mmoja…
Kilimo Biashara
Unapouza mazao yako zingatia vipimo sahihi
Wakulima walio wengi wamekuwa wakipoteza mamilioni ya shilingi kutokana na uuzaji wa mazao kwa kutumia vipimo visivyokuwa sahihi Kwa kawaida wakulima wanapoamua kufanya shughuli ya uzalishaji wa mazao huwa na malengo makubwa sana ya kufaidika kutokana na mazao hayo pindi msimu wa mavuno unapofika. Hii imekuwa ni tofauti kabisa kutokana na wakulima kuishia kupata hasara inayosababishwa na kuuza mazao yao…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2022
Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…
Utengenezaji wa jibini ngumu
Hii ni jibini aina ya cheddar ambayo asili yake ni huko Uingereza lakini kwasasa hutengenezwa katika nchi mbalimbali dunian. Hatua za utengenezaji Pima ubora wa maziwa Pasha moto maziwa kufikia nyuzi joto 65C yaache katika joto kwa dakika 30 au nyuzi joto 71.5C kwa sekunde 15 Poza maziwa kufikia nyuzi joto 22 hadi 25C Weka kimea cha mtindi (mesophilic) asilimia…
EMAS: Kirutubishi chenye matumizi mengi kwa mkulima
Mlima bora ni yule anayetumia malighafi sahihi ili kuzalisha mazao mengi yenye tija na salama kwa chakula. EMAS ni nini? EMAS Effective Micro Organisms Active Solution ni namna nyepesi ya kutengeneza bakteria wazuri ama rafiki kwa njia ya kimiminika ambacho ni rahisi kutumia na pia ni salama. Mahitaji Maziwa Fresh lita 10 Maji ya mchele lita moja Molasesi lita 10…
Uzalishaji wa malisho
Bonyeza hapa na sikiliza kuhusu malisho aina ya matete na faida zake
TUNAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KUTUMA JARIDA LA OKTOBA
Habari ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu. Ni matumaini yetu kuwa uko salama na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukutumia nakala yako ya jarida la Mkulima Mbunifu. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto kidogo zilizokuwa nje ya uwezo wetu ambazo zimepelekea kusindwa kuchapisha nakala ya mwezi Oktoba kwa wakati. Jarida hili…
Tunaomba radhi kwa kutokusikika hewani
Ndugu msikilizaji na mfuatiliaji wa vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu/SAT, tunaomba radhi kutokana na kipindi chetu kilichokusudiwa kurushwa hewasi siku ya jumamosi tarehe 30 Oktoba 2021 kutokusikika. Hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Sasa kipindi hicho cha kilimo kilichokuwa kinahusu kilimo mseto na kilimo cha mzunguko wa mazao kitarushwa upya siku ya jumamosi ya tarehe…
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…