- Binadamu, Kilimo Biashara, Usindikaji

Utengenezaji wa jibini ngumu

Sambaza chapisho hili

Hii ni jibini aina ya cheddar ambayo asili yake ni huko Uingereza lakini kwasasa hutengenezwa katika nchi mbalimbali dunian.

Hatua za utengenezaji

  • Pima ubora wa maziwa
  • Pasha moto maziwa kufikia nyuzi joto 65C yaache katika joto kwa dakika 30 au nyuzi joto 71.5C kwa sekunde 15
  • Poza maziwa kufikia nyuzi joto 22 hadi 25C
  • Weka kimea cha mtindi (mesophilic) asilimia 0.25 hadi 0.5 ya maziwa yanayotumika.
  • Pasha maziwa moto hadi kufikia nyuzi joto 30 hadi 32C
  • Acha maziwa yatulie kwa dakika 15, kisha koroga na acha kwa dakika 15 nyingine yakiwa yamefunikwa.
  • Weka rennet, koroga na hakikisha nyuzi joto ni 30 hadi 32C na acha kwa dakika 30 ili yagande.
  • Kata curd, koroga na ondoa whey theluthi moja
  • Pika curd kufikia nuzi joto 38 hadi 40C, kwa dakika 45 huku ukiendelea kukoroga
  • Ondoa whey yote
  • Rundika curd (cheddaring/matting) acha kwa dakika 15, geuza na rudia tena baada ya dakika 15
  • Saga curd kwa mikono (milling) weka chumvi kwa kunyunyizia (salting)
  • Weka kitambaa kwenye kifyatulio kisha jaza curd iliyowekwa chumvi (hooping)
  • Gandamiza curd kwa kutumia mashine maalumu kwa dakika 45, kwa hali ya kawaida vijijini gandamiza kwa kutumia kitu Kizito kwa saa 24
  • Ondoa curd kwenye kifyatulio na tumbukiza kwenye maji ya chumvi kali (brining) ya asilimia 15, kwa muda was aa 12 hadi 24
  • Ondoa jibini kwenye maji ya chumvi, halafu weka kwenye kabati ya wavu kwenye chumba kikavu chenye ubaridi na hewa ya kutosha kwa muda wa miezi mitatu
  • Paka parrafin wax au cheese wax ili kutunza ubora na baada ya mwezi mmoja jibini itakuwa tayari kwa matumizi
  • Hifadhi kwenye jokofu
  • Pima uzito wa jibini kisha fungasha tayari kwa soko
  • Andika tarehe ya kutengeneza nay a mwisho wa matumizi
  • Muda wa matumizi usizidi miezi 12 baada ya kutengeneza

Matumizi

Jibini ngumu hutumika kama kitafunwa na huliwa pamoja na vyakula vingine kama vile mkate na mbogamboga.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *