- Kilimo

Utupa: Mmea wa ajabu unaofaa kwa matumizi mengi

Sambaza chapisho hili

Utupa ni aina ya mmea unaopatikana zaidi sehemu zenye baridi hasa nyanda za juu na unastawi sehemu zenye mvua za wastani na nyingi. Mmea huu hauhimili ukame.

Utupa hukua haraka na kusambaa kama usipodhibitiwa, baadhi ya nchi mmea huu umepigwa marufuku kupanda kwa sababu ya kutishia uoto wa asili.

Matumizi

Kufukuza panya / mchwa

Mmea wa utupa ni moja ya njia za asili zinazotumika kufukuza wanyama na wadudu wa aina mbalimbali wanaoharibu mazao shambani.

Endapo shamba lako limevamiwa na panya wanaochimba ardhini, unaweza kupanda utupa kwa kuchanganya na mazao mengine.

Nafasi

Panda utupa pamoja na mazao mengine kwa umbali wa mita 3 kila upande (3m * 3m) na mpakani mwa shamba.

Baada ya kipindi cha mwaka mmoja shamba halitakuwa na mashimo ya panya wala fuko.

Njia hii pia itakuwezesha  kufukuza mchwa, kwenye majumba. Unaweza kuupanda mmea huu kwenye kingo za nyumba na mpakani, kama kuna kichuguu cha mchwa panda miche hii na kichuguu kitakufa baada ya mchwa kuhama.

Kuogeshea mifugo

Unaweza kutumia mmea wa utupa kutengenezea mchanganyiko maalumu, ambao unaweza kuutumia kuogesha mifugo ili kuwakinga na kuwaondolea maradhi ya ngozi.

Namna ya kuandaa

Chukua kilo moja ya majani ya utupa na maji lita 25, loweka kwa saa mbili mpaka tatu au chemsha kwa dakika 30 na lita 27 za maji, chuja kwa kitambaa kisha weka kwenye bomba la kuogeshea mifugo, changanya na sabuni ya unga kidogo ili iweze kunata kwenye mwili wa mnyama, na hapo inakuwa tayari kwa matumizi.

*ONYO Kamwe usitumie kuogeshea nguruwe hawana uwezo wa kuhimili dawa hii kwenye ngozi zao.

Kunyuzia shambani / bustani

Utupa unaweza kutumika kwenye mazao ya aina mbalimbali, hii ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na wadudu waharibifu na magonjwa yatokanayo na wadudu hao.

Namna ya kuandaa

Chukua kilo moja ya majani ya utupa na maji lita 5 loweka kwa saa mbili mpaka saa tatu au chemsha kwa dakika thelathini na lita 6 za maji.

Chuja kwa kitambaa kisha weka kwenye bomba na kunyunyuzia shambani au majumbani kwa ajili ya kuua wadudu kama vile mbu, mende, n.k

Kuhifadhi nafaka kwenye ghala

Chukua gramu 100 za unga wa majani ya utupa changanya na mahindi au maharagwe kilo 100, funga vizuri gunia lako na hifadhi kwenye ghala. Dawa hii huwa na nguvu kwa muda wa mwaka mzima.

Matumizi mengine

Endapo utupa utapandwa mchanganyiko na mazao mengine huongeza rutuba ardhini kwa kuongeza kiasi na naitrojeni.

Mbegu zake zinaweza kutumika kama moja ya chanzo cha protini kwenye vyakula vya mifugo, hususani mbuzi.

*Tahadhari

Usilishe kwa kiwango kikubwa kwani mbegu za utupa zina chembechembe za sumu zinazoweza kudhuru mifugo endapo zitaliwa kwa wingi.

Unga wa mbegu za utupa, unaweza kusababisha samaki wapooze (paralyze).

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

18 maoni juu ya “Utupa: Mmea wa ajabu unaofaa kwa matumizi mengi

    1. Asante sana Bonny. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu na Mkulima Mbunifu, tusiache kufanya kazi kwa pamoja ili tuweze kufikia malengo mazuri

      1. Mie nataka kujua kilimo cha parachichi in mbegu gani nzuri na muda mfupi ndio nahitaji ,, shamba LA kheka moja litagharim miche mingapi ya parachichi

        1. Habari Winfrida, asante sana kwa kuendelea kusoma na kufuatilia makala mbalimbali za Mkulima Mbunifu. Kuhusu kilimo cha parachichi kuna aina mbalimbali za parachichi za muda mfupi ambazo unaweza kulima. Mbegu aina ya Hass ni nzuri zaidi kwa kilimo cha parachichi. Kwa ekari moja ni miche kati ya 40 hadi 100 hii inategemea unahitaji kulea matunda yako kwa namna gani. Kama utahitaji iwe miti mikubwa basi utaotesha 40 ila kama hutaiacha iwe mikubwa unaweza kuongeza hadi 100

  1. Unapo tumia utupa kuhifathi mahindi itachukua mudagani ili uweze kuyatumia mahindi hayo kwa chakula??

    1. Asante sana kwa swali lako. Chukua majani 3-5 makubwa ya shubiri mwitu, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Kisha wape kuku kwa siku 5 hadi 7. Isiyotumika au inayobaki kwa siku hiyo baada ya kuku kunywa mwaga na tengeneza tena nyingine kwa muda hadi wa siku 5. Mchanganyiko huu hutibu kideri/ mdondo, sotoka, homa ya matumbo (typhoid), mafua, kipindupindu cha kuku.

    1. Hi Stella,

      Welcome to Mkulima Mbunifu and thank you for checking up with us. We received your email address and we shall be sending to you every month.

      Your warmly welcome

  2. Je, utupa ni ule mmea unaowasha ukigusa ganda la matunda yake, au ni ule unaotumika kuleweshea samaki.

    1. Habari
      Karibu Mkulima Mbunifu na asante sana kwa kuendelea kuwa miongoni mwa wadau, wafuatiliaji na wasomaji wa makala mbalimbali za jarida letu la Mkulima Mbunifu.

      Kuhusu utupa, unaweza kuanza kutumia mazao mara baada ya siku 3 na itakuwa iko salama.

      Karibu sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *