- Mifugo

Chakula rahisi kwa utunzaji wa nguruwe wadogo wanaokuwa

Sambaza chapisho hili

Nguruwe ni mnyama anaeweza kuishi sehemu za vijijini kwani mijini kule wengi huwa hawapendelei sanaana ufugaji huu. Nguruwe hubeba mimba kwa muda wa miezi mitatu na wiki mbili.

Ili kuwa na ufanisi na kwa gharama ndogo, mfugaji anapaswa kuzingatia matunzo na kufahamu njia sahihi za ulishaji wa nguruwe wadogo, ili waweze kukua kwa haraka.

Mfugaji anaweza kutumia malighafi zifuatazo ili kuweza kutengeneza chakula kwa ajili ya nguruwe wake.

Mahitaji

Haya ni mahitaji kwa uwiano wa nguruwe wadogo 100 wanaokuwa.

  • Mahindi yaliyo sagwa kilo ishirini na sita.
  • Pumba ya mahindi kilo hamsini na mbili.
  • Mashudu ya alizeti kilo kumi na tano.
  • Dagaa walio sagwa kilo nne.
  • Chokaa ya mifugo kilo mbili.
  • Pig mix nusu kilo (0.5kg).
  • Chumvi nusu kilo (0.5 kg).

Ni muhimu kukumbuka kuwa unapo wachanganyia nguruwe chakula hiki, kwa nguruwe dume akifikisha miezi sita anakuwa na kilo sitini(60) na kuendelea.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

13 maoni juu ya “Chakula rahisi kwa utunzaji wa nguruwe wadogo wanaokuwa

  1. Asante sana. Je kipimo hicho cha chakula ni kwa siku moja au muda gani? Lakini pia naweza kuweka nguruwe wadogo 100 katika banda lenye ukubwa gani?

  2. Nashukuru kwa dondoo za chakula cha nguruwe wadogo,je wanakula kiasi gani kila MMoja kwa Siku?

    1. Habari,
      Hii inategemea na uzito wa nguruwe lakini mara nyingi mara wanapoachishwa kunyonya, nguruwe mwenye uzito wa kilo 10 hadi 17 anakula chakula kilo 0.75 kwa siku yaani robo 3.

    2. Imani Hapa nimeelewa lakini je upatikanaji was hivo vyakula . pia utokaji wa bidhaa zetu no shida sana hivo uweza kuta nguruwe wa kilo 60 had 80 wanakuambia laki tatu ukilinganisha na gharama za uendeahaji inakata sana

      1. Habari, karibu Mkulima Mbunifu. Ukihitaji nguruwe wakulipe vizuri jitahidi kufuga nguruwe wengi na usinenepeshe sana nguruwe ili wasijenge mafuta mengi mwilini bali watengeneze steki na katika uuzaji jitahidi kuuza nyama na siyo nguruwe

        1. Habar mm ni mfugaji shida natumia mda mrefu mpka kuuza sasashida yangu natka nipate nenepesha nifuge kwa mda mtupi je mnazo

    1. Habari,

      Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala zetu. Unaweza kuwapata ila kwasasa tuna mawasiliano na muuzaji toka Arusha ambaye anaweza pia kukusafirishia kwa gharama mtakazokubaliana nazo.

      Wasiliana na Nelson Kessy kwa simu namba 0713 948 144

      Karibu sana Mkulima Mbunifu

  3. Nashukuru kwa maelekezo mazuri nitayafuatilia na pia ntapataje mbgu nzuri nipo mwanza

    1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida letu. Tafadhali subiri tuwasiliane na wauzaji tukupe jibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *