- Mifugo

Dondoo muhimu za ufugaji bora wa ng’ombe

Sambaza chapisho hili

Ng’ombe ni mifugo ambayo inategemewa sana na wananchi walio wengi hapa nchini. Kuna aina tatu za ng’ombe wafugwao hapa nchini ambayo ni ng’ombe wa kisasa, kienyeji, na machotara.

Zifuatazo ni faida zipatikanazo na ufugaji wa ng’ombe

  • Chakula kama vile maziwa na nyama
  • Mbolea
  • Ngozi ambayo hutumika kama malighafi kutengeneza, viatu, mikanda, mikoba, nguo na vitanda
  • Kujipatia pesa, pia ni akiba
  • Ufahari na huongeza heshima kwa baadhi ya makabila.
  • Kupata mapambo kama pembe

Uthibiti madhubuti wa magonjwa mbalimbali

Ili ng’ombe akue vizuri, akupe maziwa mengi na awe na afya nzuri zingatia yafuatayo;

  • Uchaguzi wa ng’ombe mzuri wa kufuga
  • Malisho mazuri tangia akiwa ndama
  • Banda zuri

Chakula cha ng’ombe

Chakula ni kitu muhimu kwa mifugo yote. Ulishaji  wa  ng’ombe  wa  maziwa  na  wengine  huanzia  toka  anapozaliwa  (ndama) na  ndipo  atakapo  kuwa  na  mafanikio  mazuri katika uzalishaji.

Ndama  anapozaliwa  tu  anahitaji  kupata maziwa  ya  kwanza  (colostrum)  kwa  muda usiopungua   siku   tatu   mfululizo.

Maziwa haya humsaidia kujikinga na magonjwa na pia    humpatia    ndama    virutubisho    vya kutosha.  Baada  ya  hapo  ndama  aendelee kunywa  maziwa  ya  mama  mpaka  atakapofikia   mwezi   mmoja,   aanze   kupatiwa chakula  cha  ziada  (pumba  ya  mahindi  iliyochanganywa  na  mashudu  pamoja  na majani mabichi yaliyokatwa katwa vipande vidogo vidogo).

Ndama akifikia umri kati ya miezi miwili na sita  unaweza  kumuachisha  kunyonya,  na anatakiwa  apatiwe  chakula  chenye virutubisho  sawa  na  maziwa  ya  mama.

Kwa  mfano  apatiwe  pumba  za  mahindi zilizochanganywa  na  mashudu  na  majanimabichi  (apatiwe  wakati  wote).

Ngombe jike  wa  kisasa  hufikia  umri  wa  kupandwa akiwa    na    mwaka    mmoja    na    nusu. Ng’ ombe atakapokuwa na mimba ya miezi 7  kama  alikuwa  anakamuliwa  anatakiwa kukaushwa  na  kupatiwa  chakula  chenye virutubisho zaidi.

Nyumba ya ng’ombe

Nyumba ni muhimu katika ufugaji wa ng’ombe.   Tunashauriwa   kuwahifadhi ng’ombe  katika  banda  lenye  hewa  ya kutosha,  lisilo  na  joto  kali,  lisilopitisha maji  ya  mvua  na  liwe  lenye  nafasi  ya kutosha.

Pia banda la ng’ombe liwe na sakafu   yenye   mteremko   kidogo   kurahisisha usafi wa banda na kuzuia kutuama  kwa  maji  na  mkojo.

Nyumba ya ng’ombe   inatakiwa   iwe   safi   wakati wowote ili kuzuia magonjwa mbalimbali.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

9 maoni juu ya “Dondoo muhimu za ufugaji bora wa ng’ombe

    1. Habar, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako.
      Unaposema juu yaufugaji wa ng’ombe ni kipengele gani unahitaji kujifunza kwa maana kupitia makala hii tumeandika dondoo muhimu za ufugaji bora wa ng’ombe

        1. Habari, karibu Mkulima Mbunifu.

          Unamaanisha ng’ombe wa maziwa? Fuga Friesian au Ayrshire

        2. Ni vyema ukiweka picha na aina ya ng’ombe tukajua huyu ni Aina flani na huyu ni aina flani

          1. Happy Birthday,
            Tunashukuru kwa kuendelea kufuatilia na kusoma majarida yetu. Tunashukur pia kwa ushauri wako

    1. Habari,

      Karibu sana. Unahitaji ushauri kuhusu nini hasa kwenye ufugaji wa ng’ombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *