- Mifugo

Kinga dhidi ya magonjwa

Sambaza chapisho hili

Magonjwa yaenezwayo na kupe

Ndigana kali, ndigana baridi, kukojoa damu na moyo kujaa maji.

Kinga:  Ogesha wanyama wako  kwa  kutumia dawa ya kuua kupe mara moja kwa wiki.

Magonjwa yaenezwayo na mbung’o

Ndorobo   ni   ugonjwa   mkuu   uletwao   na mbung’o

Kinga:  Wachanje ng’ombe kwa kutumia dawa iitwayo samorini kila baada ya miezi mitatu.

Magonjwa yasababishwayo na virusi

Ugonjwa wa midomo na miguu, sotoka, ndui

Kinga:   Chanjo   ya   virusi   maalum   pata ushauri wa daktari wa mifugo

Magonjwa yasababishwayo na bakteria

Chambavu, homa ya mapafu, kimeta

Kinga:  Chanjo maalum pata ushauri wa daktari wa mifugo

Lishe duni

Kudumaa, ugumba, mifupa kuwa laini

Kinga:  Lisha wanyama chakula kizuri na chenye virutubisho vya kutosha.

Magonjwa yatokanayo na mazingira

Misumari kwenye matumbo, mifuko ya plastiki, kuoza kwato

Kinga: Chambua pumba, toa misumari

Jipu la kiwele

Kinga: Usafi kwenye banda la ng’ombe, kusafisha kiwele kabla na baada ya kukamua. Mkamuaji awe msafi na kucha fupi na aoshe mikono kwa sabuni kabla ya kumkamua ng’ombe. Pata ushauri wa wataalamu wa mifugo kuhusu ugonjwa huu.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *