Katika msimu huu wa Vuli ambao huanza mwezi Oktoba, inatarajiwa kuwa joto la bahari katika eneo la tropiki ya kati ya Bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuendelea kuwa la Juu ya Wastani, hali inayoashiria uwepo wa El Niño yenye nguvu kubwa. Aidha, joto la bahari la Juu ya Wastani linatarajiwa zaidi katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi ikilinganishwa na…
Kilimo
MAONESHO YA 10 YA AFRICA AGRI EXPO 2026 YAANZA DAR ES SALAAM
Teknolojia, uwekezaji na kilimo endelevu vyapewa nafasi katika mjadala wa mustakabali wa sekta ya kilimo DAR ES SALAAM: Maonesho ya 10 ya Africa Agri Expo 2026 yameanza leo, Septemba 2, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Trade Fair Grounds, maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam, yakileta pamoja wakulima, wataalamu, watafiti, wawekezaji, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya kilimo…
Uko tayariiii??? Africa Agro Expo ni Kesho!! MKULIMA MBUNIFU TUTAKUWEPO
TUNAWAKUMBUSHA TENA! Tarehe 2–3 Septemba 2026 | Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J.K. Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania Sekta za kilimo, mifugo na usindikaji wa chakula barani Afrika zinaingia katika kipindi kipya cha ukuaji, na mwezi huu wa Septemba, wadau wakubwa wa tasnia hii watakutana chini ya paa moja jijini Dar es Salaam. Maonesho ya 10 ya Africa…
Tukio Kuu la Kilimo Barani Afrika: India Katika Sekta Inayokua kwa Kasi ya Kilimo, Mifugo na Chakula Tanzania
Usikose Tukio Kuu la Kilimo Barani Afrika
Ukiwa na wageni 10,000, kampuni 1,000, na nchi 35 zikikutana kwa siku mbili, AAE na FLIP 2026 ni miongoni mwa fursa muhimu zaidi za biashara katika kalenda ya kilimo Afrika mwaka huu.
Iwe unakuja kugundua teknolojia mpya, kukutana na washirika muhimu, au kuanzisha ushirikiano mpya wa usambazaji, uhusiano utakaoujenga Dar es Salaam unaweza kuunda biashara yako kwa miaka mingi ijayo.
Jisajili sasa ili kujihakikishia nafasi katika Tukio Kuu la Kilimo Barani Afrika: 👉 https://africa-agriexpo.com/visitor-registration.html
Tukutane Dar es Salaam, tarehe 2–3 Septemba 2026.
Umejiandaa kuhudhuria maonyesho ya wakulima maarufu kama Nanenane?
Hakika siku hazigandi, saa nayo inatembeza mshale wake kwa haraka zaidi, hatimaye sasa tumebakiza siku chache sana kuanza kwa maonyesho ya wakulima Nanenane. Kama kawaida, Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, wajasiriamali, watu binafsi na wananchi kwa ujumla wanakuandalia maonyesho ya siku nane ya kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli mbalimbali za kibishara katika kanda mbalimbali nchini. MKULIMA MBUNIFU kama…
Expo ya Kilimo ya Afrika Inakuja Dar es Salaam, Usikose!
Tarehe 2 na 3 Septemba 2026, Dar es Salaam itakuwa kitovu cha kilimo cha Afrika. Kila mwaka, wakulima, wafanyabiashara, wawekezaji, na wataalamu wa kilimo kutoka nchi mbalimbali wanakutana katika mkutano mmoja mkubwa kuzungumza biashara, kujifunza, na kuunda ushirikiano. Mwaka huu, mkutano huo unafika nyumbani kwetu, hapa Tanzania. Tarehe 2 na 3 Septemba 2026, Dar es Salaam itaandaa toleo la 10…
TUJIKUMBUSHE: Mambo ya kuepuka ili usipate hasara katika kilimo
Kwa siku za nyuma, takwimu zilionesha kuwa 80% ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo jambo ambalo kwa sasa inaonekana idadi yao kupungua na kufikia 60%. Hii huenda ikawa ni kutokana na hasara zinazopatikana kwenye kilimo. Hasara katika kilimo zimekuwa ni jambo kubwa ambalo linasumbua vichwa vya wakulima wengi ndani na nje ya Tanzania. Hasara hizi huweza kusababishwa na mambo mengi sana…
Jifunze namna bora ya ubebeshaji wa miche ya matunda mbalimbali
Ubebeshaji maana yake ni uunganishaji wa sehemu mbili au zaidi za mimea tofauti na kuwa mmea wenye shina moja. Ubebeshaji hufanyika katika mimea ya mazao ambayo yako katika jamii au ukoo mmoja kwa mfano; embe dodo na viringe, chungwa na limao, parachichi aina ya hass na la kienyeji, passion zambarau na njano, biringanya za aina tofauti, maua ya waridi ya…
Jifunze kusindika majimbi kuongeza thamani na kipato
Magimbi (yam) ni zao la mizizi lenye umuhimu mkubwa katika usalama wa chakula na kipato cha wakulima wadogo wadogo nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Ingawa halijapewa uzito mkubwa kama mihogo au viazi, magimbi yana nafasi ya kipekee katika lishe na uchumi wa vijijini. Value chain ya magimbi inahusisha hatua zote kutoka uzalishaji shambani hadi kufika sokoni na kwa mlaji…
Kwa nini miembe inadondosha maua?
Kudondoka kwa maua kwenye miembe yako inaweza kutokana na upungufu au ukosefu wa aina fulani ya madini. Virutubisho na madini kwenye miembe vinahitaji ufahamu na uelewa wa hali ya juu kwa kile kinachohitajika. Tofauti na hilo, unahitaji kuzingatia kiasi cha fosiforasi ili kuchochea uwezo wa mizizi na ukuaji wa mmea. Mkulima anatakiwa kuweka utaratibu wa kuweka mbolea kwenye mimea yake…








