Katika msimu huu wa Vuli ambao huanza mwezi Oktoba, inatarajiwa kuwa joto la bahari katika eneo la tropiki ya kati ya Bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuendelea kuwa la Juu ya Wastani, hali inayoashiria uwepo wa El Niño yenye nguvu kubwa. Aidha, joto la bahari la Juu ya Wastani linatarajiwa zaidi katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi ikilinganishwa na…
Binadamu
Tanzania yaibuka kitovu cha fursa za kilimo na uwekezaji Afrika
Tanzania imeendelea kujidhihirisha kuwa eneo lenye fursa kubwa kwa uwekezaji na biashara katika sekta ya kilimo barani Afrika, huku kampuni, wawekezaji, wakulima na wadau wengine wakikutana katika 10th Global Africa Agri Expo na 3rd Future Food and Livestock Expo yaliyofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam. Ikiwa ni siku ya pili, maonyesho hayo yameendelea kuwaweka pamoja wadau kutoka ndani…
MAONESHO YA 10 YA AFRICA AGRI EXPO 2026 YAANZA DAR ES SALAAM
Teknolojia, uwekezaji na kilimo endelevu vyapewa nafasi katika mjadala wa mustakabali wa sekta ya kilimo DAR ES SALAAM: Maonesho ya 10 ya Africa Agri Expo 2026 yameanza leo, Septemba 2, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Trade Fair Grounds, maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam, yakileta pamoja wakulima, wataalamu, watafiti, wawekezaji, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya kilimo…
Tukio Kuu la Kilimo Barani Afrika: India Katika Sekta Inayokua kwa Kasi ya Kilimo, Mifugo na Chakula Tanzania
Usikose Tukio Kuu la Kilimo Barani Afrika
Ukiwa na wageni 10,000, kampuni 1,000, na nchi 35 zikikutana kwa siku mbili, AAE na FLIP 2026 ni miongoni mwa fursa muhimu zaidi za biashara katika kalenda ya kilimo Afrika mwaka huu.
Iwe unakuja kugundua teknolojia mpya, kukutana na washirika muhimu, au kuanzisha ushirikiano mpya wa usambazaji, uhusiano utakaoujenga Dar es Salaam unaweza kuunda biashara yako kwa miaka mingi ijayo.
Jisajili sasa ili kujihakikishia nafasi katika Tukio Kuu la Kilimo Barani Afrika: 👉 https://africa-agriexpo.com/visitor-registration.html
Tukutane Dar es Salaam, tarehe 2–3 Septemba 2026.
Umejiandaa kuhudhuria maonyesho ya wakulima maarufu kama Nanenane?
Hakika siku hazigandi, saa nayo inatembeza mshale wake kwa haraka zaidi, hatimaye sasa tumebakiza siku chache sana kuanza kwa maonyesho ya wakulima Nanenane. Kama kawaida, Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, wajasiriamali, watu binafsi na wananchi kwa ujumla wanakuandalia maonyesho ya siku nane ya kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli mbalimbali za kibishara katika kanda mbalimbali nchini. MKULIMA MBUNIFU kama…
Umuhimu wa lishe ya mboga kwa afya
Mboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, mboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za mboga kwenye chakula…
Udongo ukiwa mfu hakuna uzalishaji: Lisha udongo upate mavuno bora
Ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha anauilisha udongo kwa kutumia virutubisho vya asili, ili kuweza kuwa na rutuba na kuzalisha mazao yenye tija. Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho. Vipengele…
Tukumbushane namna ya kuhifadhi malighafi na chakula cha samaki
Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda.
Je, Una swali lolote kuhusiana na ufugaji wa Samaki? Tuulize, Tukujibu
Ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa MkM kuthamini maoni yako na kujibu maswali yenu kwa kupitia wataalamu wa kada mbalimbali. Katika toleo hili Musa Said ambaye ni mtaalamu wa Samaki anaendelea kujibu maswali kuhusiana na ufugaji wa samaki. Shime, kama nawe una maswali basi usisite ili upate jibu na uondokane na dukuduku. Lai otieno anauliza: Mimi natoka Musoma mjini na…
Lishe na vyanzo asili ya chakula
Lishe bora inajumuisha aina mbalimbali za vyakula kutoka makundi tofauti ya chakula, na hutoa virutubisho na ladha tofauti. Makundi haya ni muhimu kwa afya na ukuaji wa mwili: Nafaka na mizizi: Mahindi, viazi, ndizi — hutoa wanga kwa ajili ya kuongeza nguvu. Mikunde: Maharagwe, soya — chanzo cha protini kwa ajili ya kujenga mwili. Karanga na mbegu: Njugu, korosho —…









