- Binadamu, Kilimo, Mifugo, Udongo

Maharagwe ya ngwara: Muunganiko wa lishe ya kiafrika

Sambaza chapisho hili

Ngwara ambalo pia hujulikana kama Fiwi, ni aina ya maharagwe katika familia ya Fabaceae. Asili yake ni katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na hulimwa katika maeneo ya kitropiki.

Zao hili lenye utajiri wa virutubisho, ambalo kwa muda mrefu lilisahaulika, sasa limeanza kupata umuhimu mkubwa kutoka kwa wadau wa kilimo.

Zao hili linastawi katika hali ya hewa ya joto inayofanana na maeneo ya kitropiki na subtropiki. Linajulikana kwa ukuaji wake wa haraka na uwezo wa kuzoea aina mbalimbali za udongo.

Aidha, Ngwara hutoa maua mazuri ya mapambo na mara kwa mara hulimwa kwa sababu ya uzuri wake wa mapambo.

Ngwara asili yake ni Afrika na inakuzwa na sasa inalimwa katika sehemu nyingine za dunia ikiwa ni pamoja na, Asia, Karibiani na Amerika Kusini.

Inajulikana kwa thamani yake ya juu ya lishe, kustahimili ukame na kukabiliana na hali tofauti.

Ngwara ina matumizi mengi; mbali na kuliwa na binadamu pia hutumika kama zao la malisho ya mifugo na pia inaaminika kuwa na dawa kwa baadhi ya magonjwa yakiwemo Shinikizo la damu na kisukari.

Soko la nje ni ngwara nyeusi (NMD 20) ni Kenya, soko la ndani ni ngwara nyekundu (NMD 19) hupendwa na watanzania kama maharagwe.

Faida za ngwara kiuchumi

  • Ngwara hustahimili ukame ambao huifanya kuwa zao la kuchagua wakati wa uhaba wa mvua
  • Wakulima wataweza kuwa na kipato cha uhakika
  • Kihistoria ngwara ililimwa na wanawake karibu na kaya kama zao la uhakika wa chakula
  • Inahamasisha wanawake kusindika unga wa ngwara na kutengeneza bidhaa nyingine za chakula kama mkate, biskuti n.k.
  • Uhuru wa kifedha hupunguza utegemezi wa wanawake kwa wanaume.

Faida za ngwara kiafya

  • Inatambuliwa na jamii za kitamaduni kama chakula cha chaguo la wanawake baada ya kujifungua
  • Inajulikana kuongeza uzalishaji wa maziwa, na kusaidia miili ya wanawake kupona haraka matatizo ya kuumwa mgongo baada ya kuzaa kwa sababu inaimarisha mifupa
  • Ngwara ni zao la lishe lenye protini muhimu na vitamini ambazo zinaweza kuboresha afya ya binadamu na wanyama.
  • Majani machanga ya ngwara ni mazuri kama mboga. Unachuma majani yale malaini ya juu wakati ya kuchuma na kuyakatakata na kupika kama kawaida.
  • Inaaminika kuwa ni dawa kwa baadhi ya magonjwa yakiwemo shinikizo la damu na kisukari.
  • Ngwara yanasaidia pia kuongeza virutubisho kama vile vitamin A, K na D

Kumbua: Inashauriwa wakati wa kupika ngwara kuiloweka kwanza masaa nane ili kupinguza muda wa kupikia.

Faida za ngwara kwenye udongo

  • Ngwara inafunika ardhi hivyo kuzuia mmomonyoko wa udongo.
  • Ngwara inaongeza rutuba (kilo 140/ heka) kwenye udongo hivyo kumpunguzia mkulima gharama za kununua mbolea.
  • Ngwara inasaidia pia kuzuia magugu kutokana na sifa yake ya kufunika ardhi.
  • Ngwara inasaidia kutunza unyevu kwenye ardhi kutokana na sifa yake ya kufunika ardhi.

Faida za ngwara kwa mifugo

  • Majani ya ngwara ni mazuri na yanatumika kama malisho ya mifugo.

Namna ya kupanda ngwara

  • Kitaalamu, inashauriwa kupanda ngwara kwa kipimo cha sentimeta 60 (futi mbili) kati ya shimo na shimo linguine na pia inashauriwa kupanda kwa kipimo cha sentimeta 75 (sawasawa na futi mbili na nusu) kati ya mstari mmoja na mstari mwingine. Umbali huu unatokana na sifa ya zao la ngwara kukua kwa kusambaa na kufunika ardhi.
  • Pia, kama utapanda kilimo mseto ya ngwara na mahindi, inashauriwa kutanguliza kupanda mahindi kwanza, ikikua urefu wa goti, unaweza ukapanda ngwara ili kuzuia mahindi yako yasinyongwe na ngwara ukizipanda kwa pamoja.

Ukuaji wa ngwara pamoja na mavuno

  • Ngwara nyeusi ijulikanayo kitaalam kama (NMD-19) hukua kwa siku 65 mpaka 85 na ngwara nyekundu (NMD-20) hukua kwa siku 60 mpaka 80.
  • Pia, aina hizi mbili za ngwara kiasi chake cha mavuno ni tani moja mpaka tani moja na nusu kwa eka.
  • Inahitajika kuvuna angalau mara mbili na zaidi ya mara tatu, kutegemeana na upatikanaji endelevu wa unyevu kwenye udongo. Hata hivyo, wakati wa kiangazi au katika maeneo kavu, uvunaji unaweza kufanywa mara moja kwa sababu maganda ya mbegu yanafungwa kidogo. Lakini pia katika msimu wa kiangazi au baadhi ya maeneo kavu, mazao ya ngwara yanaweza kukomaa kwani ukuaji ni mdogo, kwa hali hii uvunaji unaweza kufanywa mara moja wakati maganda yote yakiwa yamekauka.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *