- Mifugo

Mambo muhimu ya kuzingatia kwa unenepeshaji wa nguruwe

Sambaza chapisho hili

Nguruwe wanaonenepeshwa wanahitaji kutunzwa vizuri ili waweze kufikia uzito wa kuchinjwa mapema. Nguruwe waanze kunenepeshwa wakiwa na umri wa wiki 9 hadi 14 na uzito wa kilo 25 hyadi 30. Nguruwe wana uwezo wa kuongezeka uzito wa hadi gramu 700 na 800 kwa siku kuitegemeana na aina ya nguruwe na matunzo.

Nguruwe wanaweza kunenepeshwa na kufikisha uzito wa kuchinjwa yaani kilo 85 hadi 170 kutegemeana na hitaji la soko katika umri wa wiki 23 hadi 29 kutegemeana na utunzaji na aina ya nguruwe.

Ulishaji wa nguruwe wanaonenenpeshwa

Nguruwe wanaonenenepeshwa wapatiwe kiasi kidogo cha vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwani vyakula hivi hutumia nguvu nyingi katika kuvimeng’enya.

Nguruwe wapatiwe vyakula vyenye mafuta na vyakula vyenye mchanganyiko wa protini inayotokana na mime ana ile inayotokana na wanyama ili kupata viinilishe vya kutosha vinavyohitajika mwilini.

Aidha wanahitaji kupatiwa chakula cha kutosha ili kuongeza uzito kwani ongezeko la uzitohutokana na kula vyakula vya ziada. Nguruwe asipokula chakula cha kutosha atapunguan uzito. Ili aongeze uzito anatakiwa apatiwe chakula cha ziada zaidi ya kile kinachohitajika katika kuuwezesha mwili kufanya kazi.

Nguruwe wanaonenepeshwa wabadilishiwe vyakula tofauti ili kuongeza hamu ya chakula na ulaji. Pia hakikisha wanafikia chakula nak ama wanakaa wengi katika chumba kimoja hakikisha sehemu za vyakula zinatosha kwa kila mmoja kula kwa wakati. Nguruwe wapatiwe maji safi ya kunywa wakati wote.

SN Aina ya chakula Kiasi (kg) Kiasi (kg)
    Mfano Na. 1 Mfano Na. 2
1 Mahindi yaliyosagwa 25
2 Pumba za mahindi 55 60
3 Pumba za ngano/mpunga 0 20
4 Mashudu ya Alizeti 14 10
5 Mashudu ya pamba 0 5
6 Dagaa 3 3
7 Chokaa ya mifugo 2 1.25
8 Pig mix 0.5
9 Premix 0.25
10 Chumvi iliyosagwa 0.5 0.5
  Jumla 100 100

 

Ukubwa wa eneo la chumba cvha kunenenpesha nguruwe

Nguruwe anayenenepeshwa mwenye uzito wa kilo 20 hadi 45 anatakiwa kukaa kwenye chumba chenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 0.37 na walio na uzito wa kilp 46 hadi 100 anatakiwa kukaa kwenye chumba chenye ukubwa wa mita za mraba 0.84. Eneo lisipokuwa la kutosha litasababisha nguruwe kupata usumbufu na kusababisha ashindwe kula vizuri hivyo kusababisha apunguze uzito au asiongezeke kabisa.

Hakikisha chumba cha nguruwe wanaonenepeshwa kina mzunguko mzuri wa hewa ili kuweza kumkinga na matatizo katika mfumo wa upumuaji. Chumba ni lazima kiwe safi na lkinasafishwa mara kwa mara.

Joto ni muhimu liangaliwe kwani likiwa kali sana litasababisha nguruwe washindwe kula na kusababisha kupungua uzito hivyo ni muhimu kuhakikisha nguruwe hawapati usumbufu kutokana na joto kali au baridi kali.

Linda afya ya nguruwe wanaonenepeshwa

Nguruwe wanaonenepeshwa wachunguzwe afya mara kwa mara kwani nguruwe mgonjwa hushindwa kula vizuri na hutumia kiasi kingi cha vitamini na viinilishe vingine kupambana na ugonjwa. Endapo ataonyesha dalili za ugonjwa toa taarifa mapema kwa mtaalamu wa mifugo.

Aidha, nguruwe wanaonenepeshwa wapatiwe dawa za minyoo kila mwezi kwani minyoo hupunguza upatikanaji wa viinilishe vinavyohitajika mwilini.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika ufugaj wa nguruwe

Usafi wa chumba, vifaa na mazingira ni muhimu kila siku. Chumba kiwe na vitu vya kuchezea kama vile minyororo, matairi ili kuwapa nguruwe mazoezi na kupunguza kupigana.

Endapo mfugaji atahitaji nguruwe kwa ajili ya kuzalisha, wakati mzuri wa kuchagua ni wanapofikisha umri wa miezi mitatu na kuendelea.

Nguruwe wanaweza kuchinjwa kwa ajili ya nyama wakiwa wamefikia uzito wa kilo 60 hadi 90 na ikiwa watatunzwa vizuri watafikia uzito huo wakiwa na umri wa miezi 6 hadi 9.

 

 

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

1 maoni juu ya “Mambo muhimu ya kuzingatia kwa unenepeshaji wa nguruwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *