- Kilimo, Udongo

Tengeneza mbolea ya chai ya alizeti pori (Tithonia diversifolia)

Sambaza chapisho hili

Alizeti pori maarufu kisayansi tithionia diversifolia ni aina ya mmea unaomea karibu kila mahali kando ya barabara na hata kwenye kingo za mito katika ardhi isiyokuwa na rutuba au hata katika maeneo ya bustani.

Mmea huu ni mrefu na una mashina mengi kuanbzia sehemu ya chini hadi sehemu kunakotoa maua. Kwenye udongo wenye rutuba, mmea huu huweza kufikia urefu wa mita nne (yaani futi 13).

Chai inayotengenezwa toka kwenye mmea huu imethibitika kuwa mbolea nzuri inayofaa kuweka kwenye udongo usiokuwa na rutuba. Mbolea yake ikitumika kwenye bustani ya mboga kama vile kabichi, sukuma wiki, nyanya, pilipili hoho na hata biringanya husitawi vizuri.

Sehemu zote za mmea huu hutumika kutengeneza chai lakini pia unakuwa bora zaidi kama ukitumika pale ambapo mmea umekuwa na rangi ya kijani iliyokolea zaidi na urefu wa kati ya sentimita 60 hadi 120 yaani futi mbili hadi nne na wakati ambapo bado haujaanza kutoa maua.

Namna ya kutengeneza chai ya mmea

  • Chukua majani mengi na ya kutosha kulingana na wingi wa mbolea ya chai unayohitaji kisha katakata vipande vidogo.
  • Weka majani haya katika gunia yaani kilo 50 za majani kwa kila pipa moja, jaza vizuri kwenye gunia/mfuko kisha funga kwa Kamba.
  • Jaza maji kwenye pipa hadi robo tatu kisha ning’iniza mfuko ndani ya maji kwa kufungia kwenye ufito imara ulioweka kutoka upande mmoja wa pipa hadi mwingine.
  • Funika pipa ili kuzuia naitrojeni iuspotee hewani kwa njia ya mvuke.
  • Acha kwa siku 14 hadi 21
  • Katika muda huu, utatakiwa kukoroga mchanganyiko ulioko ndani ya pipa kila baada ya siku 3 au 5 kwa kuinua mfuko kwa kiasi juu na kushusha ndani ya maji mara kadha wa kadha kwa kutumia ufito.
  • Baada ya majuuma mawili au matatu, maji yatakuwa yamebadilika rangi na kukolea na virutubisho vingi vitakuwa vimeyeyuka ndani ya maji.
  • Ondoa mfuko toka kwenye pipa tayari kwa matumizi.

Matumizi

Zimua mbolea ya chai kwa kuweka vipimo viwili vya maji kwa kila kipimo kimoja cha chai. Lakini ikiwa imekolea rangi sana basi tumia vipimo vityatu vya maji kwa kipimo kimoja cha chai.

Nyunyizia mazao kwa mchanganyiko huu ukiweka kwenye mashina na siyo kwenye majani mara mbili hadi tatu kwa wiki kwa wiki tatu hadi nne.

Tumia chai hii kwenye mimea yote inayohitaji mbolea ya naitrojeni na yenye upungufu nkama bvile mimea inayoonekana kudumaa, kuinama, kufifia, yenye majani ya cjano au yenye majani inayoonekana kutokuumbika vizuri.

Kumbuka: Unaweza pia kutumia majani ya komfri (Symphytum officinale) badala ya alizeti poro kutengenezaz mbolea ya chai kwa uwiano huu huu

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *