- Kilimo

Mmea wa artichoke na faida zake kwa mwanadamu

Sambaza chapisho hili

Mimea mingi ina faida katika mwili wa binadamu, wanyama na hata mingine kutumiwa kurutubisha udongo. Wengi wetu tumezungukwa na mimea ambayo hatufahamu faida
zake, kumbe mimea hiyo ni tiba kwa magonjwa mbalimbali hata yale sugu kama presha na mengineyo. Katika makala hii tutaangazia mmea unaoitwa artichoke.

Mkulima Mbunifu katika jitihada zake za kutembelea wakulima ilikutana na mkulima Bwana Kambaga kutoka katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Mkulima huyu anafanya kilimo biashara na analima mazao mbalimbali katika bonde la Lukozi huko Lushoto.

Mazao anayozalisha ni pamoja na kabichi nyekundu, kabichi nyeupe, saladi laini, caroti, zuchini, letusi, spinachi, koli flawa, brokoli, pilipili hoho na mazao mengine kama hayo. Pia, viungo kama seleri. Katika pitapita shambani kwa Bwana kambaga, palionekana mmea ambao ulikua umepadwa katika kingo za bustani za mboga mboga. Maswali yalianzia hapo, je mmea huu kunani?

MkM ilifanya mahojiano na Bwana Kambaga kutaka kujua mmea huu kinaga ubaga, ili kunufaisha wakulima wengine. Bwana Kambaga, alitaja jina la mmea huo kutambuliwa kamaArtichoki.

Kuhusu Artichoke
Artichoke ni mmea dawa kutoka katika familia ya mimea aina ya Asteraceae. Mmea huu hukua karibu kila mahali bila kuhitaji maji mengi, pia ina virutubisho muhimu kutumika kama dawa. Isitoshe, ikiwa unataka kuwa na mfumo thabiti wa kinga, inapendekezwa upate mbegu au miche michache na uendelee kuyakuza.

Kupanda

  • Unaweza kusia mbegu katika trei za kuoteshea,
  • Funika na matandazo, hakikisha unaifanya leya ya matandazo kua nyembamba,
  • Weka kivulini na mwagilia maji asubuhi na jioni.
  • Ndani ya siku saba (7) hadi kumi na nne (14) mmea wako utakua umeota.
  • Mimea hio ikifika sentimita tano (5) hadi (10) unaweza kuamisha katika kitalu, ama unaweza kupanda pembezoni mwa kitalu cha mboga nyingine.
  • Hakikisha unatenganisha mche mmoja na mwingine kwa sentimeta tisini (90).

Wadudu na dawa
Mmea huu unaweza kushambuliwa na nzi weupe au konokono. Unashauriwa kuzingatia dawa hai ili kudhibiti uharibifu.

Virutubisho
Mmea huu una virutubisho kadhaa muhimu katika mwili wa binadamu. Kuna madini ya fosforasi, magnesiamu, potasiamu, na chembechembe za madini ya chuma na zinki. Kuna mafuta kidogo katika artichoke, ndio sababu mboga hiyo inathaminiwa na wapenzi wa lishe na tiba asili.

Faida ya Artichoke

Wanasayansi wa kisasa wamethibitisha faida za mmea huu. Utafiti umebaini mmea huu umesaidia katika;
Kuchochea kazi ya ini, figo, kusafisha viungo.

  • Husaidia kuondoa sumu pia hupunguza (nini?) mwili.
  • Artichoke ni kichocheo kikubwa cha kusaga chakula.
  • Mimea hupunguza viwango vya sukari kwa ufanisi kwa kuongeza idadi ya bakteria wa matumbo ambayo husaidia kazi ya tumboni.
  • Na cynarin inawajibika kwa kuchochea utenda kazi wa ubongo.

Na kutokana na mabadiliko mazuri ya ndani, hali ya misumari, ngozi, na nywele pia inaboresha.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *