Hivi sasa nchini wakulima wanazalisha matunda na mbogamboga kwa wingi na katika maeneo mengi. Hii ni kwa sababu wanatambua jukumu lao katika kuongeza mapato yao ya kilimo na ustawi wa familia kama lengo la shughuli zao za kilimo. Hivyo ni muhimu wazalishaji kuhakikisha hawakosi mifumo mizuru kwa ajili ya mazao yao. Ni muhimu wakulima kuhakikisha kunakuwepo na mifumo mizuri ya…
Kilimo Biashara
NANE NANE 2022, UNAKOSAJE MAONYESHO HAYA, MKULIMA MBUNIFU KAMA KAWAIDA YETU TUTAKUWEPO KUKUJUZA KUHUSU KILIMO NA UFUGAJI
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, nane nane hiyoo imekaribia. Nchini Tanzania, kila mwaka, wakulima na wafugaji hujumuika kwa pamoja kwa muda wa siku takribani kumi kuadhimisha sikukuu ya wakulima nchini. Sherehe hizi hufikia kilele siku ya tarehe nane mwezi wa nane. Katika kipindi hiki wadau mbalimbali wa kilimo, huandaa mazao na bidhaa mbalimbali za kilimo kwa ajili kushirikisha bunifu mbalimbali na…
Matumizi mbalimbali ya mlonge
Kusafisha maji I. Kusanya mbegu za mlonge zilizokomaa kisha zimenye kupata kiini II. Twanga kiini mpaka upate unga III. Weka gramu 2 (vijiko viwili vya chai) za unga wa mlonge kwenye maji kiasi (nusu lita) natikisa kwa muda ilikupata mchanganyiko mzuri IV. Changanya kwenye maji lita 20 na koroga sana kwa muda wa dakika 10-15 V. Yaache maji yatulie kwa…
Maswali toka kwa wasomaji wa Mkulima Mbunifu kwa njia ya simu
Ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu, ni furaha yetu kuwa umeendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali zinazochapishwa kwenye jarida hili. Pia tunashukuru wewe uliefatilia na kutaka kufahamu kwa undani kwa kuuliza maswali pale ambapo hujaelewa ama umekwama. Pia tunashukuru kwa mchango wako katika kutekeleza kilimo hai. Katika makala hii ni baadhi tu ya maswali yaliyoulizwa na wakulima wasomaji wa…
Tushirikiane kupata soko la mazao ya kilimo hai
Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai. Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwenda, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali…
Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula
Upotevu wa chakula hutokea katika wigo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji. Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi. Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla ya chakula kumfikia mlaji. Kwani chakula…
Kanuni ya haki na uangalizi katika misingi ya kilimo hai
Kama ambavyo maandalizi sahihi hufanyika katika shughuli yeyote ya kimaendeleo, katika kilimo hai pia kanuni ya haki na usawa pamoja na uangalizi visipozingatiwa vyema mkulima hawezi kufaidika na kilimo hai. Kanuni ya haki na usawa Kilimo hai sharti kizingatie msingi wa mahusiano yatakayohakikisha usawa katika mazingira na fursa ya kuishi.Usawa unaojali na kuzingatia heshima, haki na kujituma kwa kila mmoja…
Unapouza mazao yako zingatia vipimo sahihi
Wakulima walio wengi wamekuwa wakipoteza mamilioni ya shilingi kutokana na uuzaji wa mazao kwa kutumia vipimo visivyokuwa sahihi Kwa kawaida wakulima wanapoamua kufanya shughuli ya uzalishaji wa mazao huwa na malengo makubwa sana ya kufaidika kutokana na mazao hayo pindi msimu wa mavuno unapofika. Hii imekuwa ni tofauti kabisa kutokana na wakulima kuishia kupata hasara inayosababishwa na kuuza mazao yao…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2022
Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…
Utengenezaji wa jibini ngumu
Hii ni jibini aina ya cheddar ambayo asili yake ni huko Uingereza lakini kwasasa hutengenezwa katika nchi mbalimbali dunian. Hatua za utengenezaji Pima ubora wa maziwa Pasha moto maziwa kufikia nyuzi joto 65C yaache katika joto kwa dakika 30 au nyuzi joto 71.5C kwa sekunde 15 Poza maziwa kufikia nyuzi joto 22 hadi 25C Weka kimea cha mtindi (mesophilic) asilimia…









