Fanya Juu ni kingamaji ambalo linachimbwa upande wa chini wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa juu wa shamba ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji ya mvua shambani na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mimea. Mwishoni inasaidia kuijanisha ardhi yako! HATUA 1: Angalia Baini uelekeo wa mtiririko wa maji katika shamba lako kwa kuangalia au kwa kutumia vipimo. •…
Mbogamboga
Ni muhimu kuzingatia soko la mazao kabla ya uzalishaji
Suala la soko ni la msingi na ni la wakati wote, kuanzia kipindi cha utafutaji taarifa ya zao husika, wakati zao likiwa katika hatua ya awali ya uzalishaji na hata linapokuwa tayari kwenda sokoni. Ni muhimu kwa mkulima kutafuta soko la mazao yake ili aweze kuuza kwa bei iliyopo sokoni na ikiwa bei imeshuka kwa ghalfa bila kutarajiwa, aweze kufikiri…
Nyuzinyuzi ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu
Nyuzinyuzi hupatikana kirahisi kwa familia kwa wakulima. Hii ni pamoja na nafaka zisizokobolewa,njugu karanga, kunde, matunda na mboga. Ni chanzo muhimu cha chakula kwa bakteria chenye faida kwenye utumbo. Inaweza kusaidia kudhibiti uzito na kupunguza hatari kwa ugonjwa wa moyo. Nyuzinyuzi (Roughage) Roughage, pia inajulikana kama nyuzinyuzi, ni sehemu ya wanga ya mimea ambayo haiwezi kumeng’enywa na mwili wa binadamu.…
Fursa ya kibiashara kwa misingi ya Kilimo hai
‘’Mimi ni mkulima wa mfano, ninazalisha mazao mbalimbali kwa misingi ya kilimo hai na nimefaidika sana’’. Hayo ni maneno ya mkulima wa kilimo hai, Bw. Michael Laizer (73), toka Kijiji cha Emaoi, Ngaramtoni, mkoani Arusha ambaye anajishughulisha na uzalishaji wa mazao ya biashara kwa misingi ya kilimo hai. Bw. Laizer, ambaye jina la kibiashara linalotambulika kama nembo kwenye bidhaa zake…
Mkulima atumia kilimo hai kujiendeleza baada ya kustaafu
“Naitwa Felister Mangalu (64) mkulima wa kilimo hai. Nilikua mfanyakazi wa serikali na nikastaafu mwaka wa 2019. Kabla ya kustaafu nilikuwa nikijiuliza maswali kuhusu nini nitafanya ili kuendelea kujikimu kimaisha endapo muda wangu wa ajira ukiisha. Najua hili ni swali ambalo watu wengi hujiuliza wakiwa na sababu kama zangu. Hata hivyo, najua tumejaliwa vipawa mbalimbali na tuna uwezo tofauti tofauti.…
Soko la mazao ya kilimo hai Tanzania
Ingawa taasisi nyingi zinasisitiza kilimo hai nchini Tanzania, kuna walaji wachache sana walio na uelewa wa bidhaa za kilimo hai. Soko la mazao ya kilimo hai lipo tu na kufahamika katika miji mikubwa kama vile Dar es Salaam na Arusha, na mashirika machache yaliyoidhinishwa katika kuuza mazao kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya soko la ndani na hata…
Bustani ya nyumbani inaweza kukukwamua kiuchumi na kuboresha afya yafamilia
Bustani ya nyumbani, ni eneo dogo lililokaribu na nyumba linaloandaliwa na wanafamilia na kupandwa mazao mbalimbali ya mbogamboga kwaajili ya familia. Hata hivyo, katika maeneo mengi wanawake ndio wamekua wakijishughulisha na bustani ndogo za nyumbani. Mara nyingi bustani ya nyumbani hujumuisha uzalishaji wa mazao ya muda mfupi hasa mbogamboga kwani ni rahisi kuyahudumia kwa gharama nafuu lakini pia yanazalisha kwa…
Ahamasika kufanya kilimo hai baada ya kusoma jarida la MkM
‘’Nimejifunza mambo mengi toka jarida la Mkulima Mbunifu hasa kuzalisha kwa misingi ya kilimo hai na nimeweza kutekeleza kwa vitendo ili wengine wajifunze kutoka kwangu”. Hayo ni maneno ya Bw. Kastuli Paulo toka kijiji cha Tumati, Wilaya ya Mbulu (Arusha), mkulima wa kilimo hai ambaye anajishughulisha na uzalishaji wa mazao mbalimbali kama vile viazi mviringo, mboga za majani ikiwamo chainizi,…
Athari za kuzidi kwa matumizi ya vitamini A mwilini
Vitamini A ni mchanganyiko wa vyakula tofauti pamoja na baadhi ya matunda. Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha ilikupata vitamin A ya kutosha katika mlo wake kila siku, ilikuongeza kinga ya mwili, kuongeza uwezo wakufikiri na kupunguza hatari ya magonjwa. Ni kwa namna gani Vitamini A inatufanya tuwe na afya iliyobora?…
Liki (leek) moja ya mazao ya mboga yasiyoshambuliwa na magonjwa
Ni vyema kuchagua aina ya mazao ambayo hayana gharama kubwa kuzalisha, wakati huo huo yakiwa na faidi kubwa. Kwa mtindo huo utaweza kupata faida ya kutosha. Liki ni moja ya mazao ya mbogamboga, ambayo yanapata umaarufu mkubwa nchini Tanzania, kutokana na kuzalishwa katika maeneo mengi, na kuwa na soko la uhakika. Zao hili ni moja kati ya mazao ya mboga…








