Hupunguza uchafuzi wa mazingira Kila siku watumiaji wa vyombo vya usafiri hubadilisha matairi. Mbali na kuwa matairi hutumika kutengeneza vitu kama viatu, mipini ya mapanga n.k, pia matairi yanaweza kutumiwa katika kilimo cha mbogamboga na matunda badala ya kuchoma matairi na kuzalisha kemikali zenye sumu kwa binadamu. Ni rahisi kutumia Ukilinganisha na kulima kwa kutengeneza matuta ya mbao au mawe,…
Mbogamboga
Fahamu ukubwa wa soko la bidhaa za kilimo hai
Historia inaonesha miaka ya zamani kilimo kilikuwa kinafanyika kupitia mbegu za mkulima mwenyewe. Hali hiyo ilitokea kutokana na utaratibu au utamaduni ambao wakulima walirithi kwa mababu kuwa mbegu, mbolea na viuatilifu vya msimu ujayo vinatoka shambani na si kwingineko. Ujio wa mapinduzi ya viwanda duniani unatajwa kuwa ulikuja na faida na hasara zake ambapo moja ya sekta ambayo imepata hasara…
Mahitaji ya uzalishaji wa mbogamboga
Mbegu Kwa matokeo mazuri ikiwemo ukuaji mzuri wa mbogamboga na mavuno mengi mkulima anashauriwa kutumia mbegu bora zilizothibitishwa. Mbegu hizo huwa na sifa zifuatazao: Hutoa mavuno mengi ya kiwango bora. Zina uwezo mkubwa wa kuota. Huhimili baadhi ya wadudu na magonjwa. Hukua kwa haraka, kwa usawa na ni imara. Ikolojia ya Eneo Eneo linalofaa kwa uzalishaji wa mbogamboga za majani…
Umuhimu wa mboga kiafya
Mboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, mboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za mboga kwenye chakula…
Faida za chaya kiafya
Amedeus Willium anauliza: Naomba kuuliza faida za chaya kwenye mwili wa binadamu Mkulima Mbunifu: Majani ya chaya ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma, protini, kalshiamu, Vitamini A, C, foliki, asidi na Vitamini B. Protini: Inajenga misuli. Mlo mmoja tu wa chaya ni sawa na kiwango cha protini kinachopatikana kwenye yai. Madini ya chuma: Kwa afya ya damu na nguvu…
Lishe ya mbogamboga ni muhimu kwa afya
Mbogamboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, Mbogamboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mbogamboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za Mbogamboga kwenye chakula…
Tumbaku kwenye mbogamboga
Tumbaku ni dawa ya asili inayoweza kutumika katika kilimo cha mbogamboga Tumia ugoro au chemsha miche 20 ya tumbaku. Dawa hii inazuia wadudu wanaoshambulia mahindi shambani, wadudu wanaokata miche, kupe, vidukari, viwavi na wengine. Chukua gramu 500 za tumbaku, changanya maji lita nane na uchemshe. Chuja baada ya kupoa, ongeza maji lita nane tena na gramu 60 za sabuni ili…
Dawa za asili kwa uzalishaji wa mbogamboga
Uzalishaji wa mboga mara nyingi unahusisha matumizi ya viuatilifu vyenye kemikali. Baadhi ya wakulima hawawezi kumudu gharama kubwa za viuatilifu hivi, ambavyo visipotumika vizuri huweza kuleta madhara, kama kuharibu mazingira, mimea na kuathiri watumiaji wa mboga. Njia asilia za kudhibiti visumbufu hutumia dawa zinazotokana na mimea ambayo hupatikana katika maeneo ya wakulima. Matumizi ya dawa hizi ni njia mojawapo ya…
Tumia mitego kunasa wadudu wkenye matunda na mboga
Kutengeneza mitego mwenyewe Ili kutengeneza mtego wa kunata, sambaza petroleum jeli au oili chafu kwenye mbao laini, iliyopakwa rangi ya njano (ukubwa wa sm 30 kwa sm 30). Weka mitego karibu na mimea lakini ikae mbali kidogo kutoka kwenye shina ili kuzuia majani yanayoanguka yasinase kwenye bodi. Chukua tahadhari kwamba rangi ya njano huvutia aina nyingi za wadudu, wakiwemo wadudu…
Kilimo bustani huongeza pato nyumbani
Kilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo. Kilimo cha bustani ni chanzo cha ajira na pato kwa wakulima na watu wengine. Mboga na matunda vinatupatia virutubisho vya kujenga, kutia nguvu na kulinda mwili. Unapowaangalia wakulima utagundua wengi wamejikita katika uzalishaji wa mazao ya bustani, kwa lengo la kukidhi mahitaji…








