- Kilimo, Mimea

Ijue Mbinu ya Kilimo Ikolojia Fanya Juu Fanya Chini

Sambaza chapisho hili

Fanya Juu ni kingamaji ambalo linachimbwa upande wa chini wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa juu wa shamba ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji ya mvua shambani na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mimea. Mwishoni inasaidia kuijanisha ardhi yako!

HATUA 1: Angalia Baini uelekeo wa mtiririko wa maji katika shamba lako kwa kuangalia au kwa kutumia vipimo.
• Fikiria sehemu ambayo ungependa kuweka Fanya Juu au Fanya Chini ili kuzuia mtiririko wa maji.
• Kwa kawaida, huwa kuna umbali wa mita 10 mpaka 20 kati ya kingamaji moja la Fanya Juu au Fanya Chini na kingamaji lingine kulingana na kasi ya mteremko. Idadi na mpangilio wa makinga maji hupatikana wakati wa upimaji.
• Hakikisha angalau una kingamaji moja upande wa juu wa shamba lako na lingine upande wa chini ya shamba lako, lakini idadi hii yaweza kuongeza kulingana na kasi ya mteremko.
HATUA 2: Pima na chora mistari kwenye ardhi. Tumia vifaa vya kupimia na uchore mistari kwenye ardhi sehemu ambayo utachimba Fanya Juu au Fanya chini ili kuzuia mtiririko wa maji.
HATUA 3: Tafuta watu wakusaidie kuchimba. Kwa mfano unaweza kutengeneza kikundi cha watu wanaoweza kushirikiana kuchimba makingamaji: kikundi kifanye kazi katika shamba la mwanakikundi mmoja hadi pale kila mwanakikundi atakapokuwa na makingamaji katika eneo lake au unaweza kuajiri watu wakufanyie kazi/kutumia mashine ya kuchimba: ni njia ya uwekezaji kwa sababu makingamaji yataongeza mavuno na kukupa kipato zaidi.
HATUA 4: Chimba makingamaji.
• Kila kingamaji linatakiwa kuwa na upana wa sentimita 60 na kina cha sentimita 60.
• Chimba kingamaji na kila baada ya mita kumi acha banio lenye urefu wa mita moja.
• Katika eneo la upande wa juu wa shamba lako chimba Fanya Chini; weka udongo uliochimbwa upande wa chini ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kuzuia maji kutoka mlimani.
• Katika eneo la chini la shamba lako chimba Fanya Juu; weka udongo uliochimbwa upande wa juu ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji na udongo ndani ya eneo lako; hii italeta mazingira mazuri kwa mazao yake.
HATUA 5: Imarisha matuta. Panda nyasi au mimea mingine yenye mizizi yenye nguvu kwenye tuta.
HATUA 6: Tunza makinga maji. Hakikisha unakagua makingamaji katika kipindi cha kuandaa shamba na kipindi cha mavuno. Kila mwaka toa udongo ulioingia ndani ya kingamaji.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na WAYDER PETER, Afisa kilimo wilaya ya Karatu kwa simu namba 0767395534

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *