- Binadamu, Kilimo

Athari za kuzidi kwa matumizi ya vitamini A mwilini

Sambaza chapisho hili

Vitamini A ni mchanganyiko wa vyakula tofauti pamoja na baadhi ya matunda. Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha ilikupata vitamin A ya kutosha katika mlo wake kila siku, ilikuongeza kinga ya mwili, kuongeza uwezo wakufikiri na kupunguza hatari ya magonjwa.

Ni kwa namna gani Vitamini A inatufanya tuwe na afya iliyobora?

  • Inasaidia ukuaji na ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu na ubongo.
  • Inasaidia macho kuona vizuri hasa wakati wa usiku.
  • Inaukinga mwili wako na magonjwa na kusaidia kupona haraka.
  • Inasaidia kuimarisha mifupa, maneno, ngozi na viungo vya ndani kama utumbo na mapafu.

Vyakula vinavyompatia mwanadamu vitamin A

Mboga za kijani iliyokolea kama: mchicha, matembele, sukumawiki, majani ya maboga na majani ya mlonge.

Mboga za rangi ya njano na nyekundu kama: Maboga, viazi vitamu vya rangi ya njano na karoti.

Matunda ya rangi ya njano na nyekundu kama: Maembe yaliyoiva, fenesi na mapapai lililoiva.

Mazao ya wanyama: Mfano nyama nyekundu, maini, figo, samaki na mayai hutupatia vitamin A.

Ilikupata Vitamini A ya kutosha katika mlo wako: inatakiwa kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha kila siku. Hakikisha unachagua mboga zenye rangi mbalimbali (kijani, nyekundu, njano)

  • Kwa watoto wachanga chini ya miezi sita hupata vitamin A kutoka kwenye maziwa ya mama.
  • Kuchanganya kiasi kidodgo cha nyama au samaki, maboga, au mboga za majani kwenye chakula cha mtoto huongeza kiwango cha vitamin A kwa watoto wenye umri zaidi ya miezi sita.
  • Watoto wale mboga na matunda ikiwezekana mara 2-4 kwa siku.
  • Vijana na watu wazima wale mboga na matunda ya kutosha kila siku.
  • Akina mama wajawazito wanatakiwa kula kiasi kikubwa cha vyakula vyenye vitamin A kila siku.

Athari za upungufu wa vitamini A

  • Kushindwa kuona vizuri hasa kunapokuwa na giza au mwanga hafifu.
  • Ngozi kukauka au kupauka na wakati mwingine kuwa na vidonda huku nywele zikikosa afya.
  • Kupata maambukizi ya magonjwa mara kwa mara hasa katika mfumo wa njia ya hewa na mfumo wa mkojo.
  • Watoto wadogo kuugua surua kwa urahisi.
  • Kudumaa kwa watoto kutokana na kukoma kukua na kuongezeka uzito.
  • Ukuaji wa taratibu na wenye kasoro wa mifupa na meno.

Athari za kuzidi kwa matumizi ya vitamini A mwilini

Virutubisho vya vitamini A vikizidi mwilini navyo huweza kupeleka athari mbalimbali kama ifuatavyo;

  • Kuhisi kizunguzungu pamoja na kichefuchefu.
  • Kuhisi maumivu ya kichwa pamoja na mzio.
  • Maumivu ya viungo na mifupaKupoteza fahamu.
  • Mtoto aliye tumboni kuumbika kimakosakama mama mjamzito akizidisha matumizi ya dawa zenye vitamini A.
  • Kunyonyoka nywele.
  • Udhaifu wa mifupa ambapo huweza kupelekea kuvunjiakwa urahisi.
  • Kukosa usingizi.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *