Wanyama walio wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa msaada kwa wakati pale maradhi yanapowakumba. Katika Makala zilizopita tuliandika juu ya sifa za mnyama mwenye afya na katika toleo hili tumeona vyema kurudia kuchapisha mada hii ili kuwasaidia wafugaji wengi ambao mara nyingi wamekuwa wakipoteza wanyama kwa ghafla bila kujua tatizo limetokana na nini. Mfugaji mzuri anatakiwa kujua nini kwa…
Mifugo
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Ufugaji holela wa kuku haufai na ni hatari
Nimekuwa mfugaji wa kuku kwa kipindi cha miaka mingi sana, tatizo ni kwamba kuku wangu hawana banda maalumu na hukutana nao jioni tu wanapoingia jikoni, na kutoka asubuhi, nimesoma kidogo kwa jirani yangu aliekuwa na Mkulima mbunifu juu ya ufugaji wenye tija, je nikianza haitanigharimu sana kwa kuwa wao hujitafutia chakula wenyewe?-Haule, Iringa. Kuku kama ilivyo kwa mifugo wengine, wanahitaji…
Fahamu ugonjwa wa ukurutu na namna ya kuudhibiti
Ukurutu ni ugonjwa wa ngozi ambao huambukizwa kwa njia ya kugusana kati ya mnyama aliyeathiriwa na aliye mzima. Kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kwa jina la menji (Mange) na husababishwa na utitiri ambao kitaalamu wanaitwa mange mites. Wadudu hawa hujikita kwenye ngozi na kufanya ngozi kuwa ngumu kama yenye magaga, kumfanya mnyama kuwashwa na mwisho manyoya kupukutika na kuondoka kabisa.…
Usafi hukinga mifugo dhidi ya ugonjwa wa ngozi
Wafugaji walio wengi, hudhania kuwa wanyama hawana hadhi ya kufanyiwa usafi au kuwekwa katika mazingira safi kama ilivyo kwa binadamu. Hata kama viwango hutofautiana, lakini ifahamike kuwa mifugo pia inastahili kuishi katika mazingira ambayo ni safi na salama. Kwa kufanya hivyo, itasaidia kuepusha wanyama kushambuliwa na magonjwa ya aina mbalimbali ikiwepo magonjwa ya ngozi yanayosababishwa na vimelea vinavyotokana na uchafu.…
Fahamu zao la sumu ya nyuki na uvunaji wake
Nchini Tanzania na maeneo mbalimbali barani Afrika, kumekuwa na ufugaji wa nyuki kwa ajili ya uvunaji wa mazao yake ili kujipatia fedha. Nyuki huvunwa mazao sita ambayo ni Asali(Honey), Nta (Wax), Chavua (Pollen), Gundi ya nyuki (Propolis), maziwa ya nyuki (Royal Jerry) pamoja na Sumu ya nyuki (Bee Venom). Lakini wafugaji wengi wamekuwa wakihagaika zaidi na zao la Asali na…
Fuata vidokezo kuhusu uuzaji wa mifugo ili kupata bei ya juu
Wafugaji wengi hawaelewi mienendo ya soko la mifugo. Wanaishia kuuza wanyama kwa bei ya chini wakati wanyama wale wale wangeweza kupata bei nzuri ikiwa mfugaji angekuwa mvumilivu na kuchukua muda kuelewa mwenendo wa soko na kuzingatia kanuni muhimu za uuzaji. Usifanye mauzo ya wanyama wachache na ya muda mfupi au kushtukiza. Hii ni kwa sababu mauzo yasiyo rasmi ni njia…
Boresha mikakati ya kutunza ng’ombe wa nyama
Tanzania ina uwezo mkubwa wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama jambo ambalo linaweza kupelekea wakulima wadogo kupata fedha ikiwa watafanya usimamizi wa hali ya juu kuzalisha nyama kwa muda mfupi. Hata hivyo, malisho na maji bado ni changamoto kwa ufugaji wa ng’ombe wa nyama nchini kwani nyasi huwa nyingi wakati wa msimu wa mvua na hupunguka wakati wa kiangazi. Ili…
Umuhimu wa kuokoa makundi ya nyuki wadogo
Nyuki wadogo huitwa kwa jina maarufu la nyuki wasiouma. Nyuki hawa wana umbo dogo kulinganisha na nyuki wanaouma lakini pia kila kabila katika Tanzania huwa na majina yake kama nyori, mbuyaa, mpunze, n.k. Mzinga uliotegeshwa katika tundu wanaoingilia nyuki wadogo ardhini kwa lengo la kuwaokoa toka ardhini kuingia kwenye mzinga huo. Nyuki hawa pia hutofautiana kulingana na meneo wanayopatikana. Wapo…








