Shule ya Sekondari Shambalai ‘‘Tuna furaha sana kukutana na Mkulima Mbunifu katika utoaji wa elimu kwani tuna bustani yetu tuliyoianzisha kwa msaada wa mwalimu mkuu, na tumeshindwa kuiendeleza kwa muda mrefu sasa kulingana na kuwa kila tulichokuwa tukijaribu kuotesha tulikosa mavuno lakini jarida hili limetupa nguvu ya kuanza kwa upya.’’ Hayo ni maneno ya mmoja wa wanafunzi wa shule hii…
Mifugo
Ufugaji wa Sungura: Aina mpya ya ujasiriamali wenye tija kwa mfugaji
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na unamuda wa kuwahudumia wanyama hawa. Ufugaji wa sungura si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa. Sungura wanahitaji uangalizi hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu. Mabanda Kuna aina mbili ya mabanda ya kufugia: • Kwanza ni mabanda ya kufugia ndani muda…
Punda anahitaji kutunzwa kama mifugo mingine
Punda ni mnyama anayefugwa na wengi lengo likiwa kutumika kutoa msaada wa nguvu kazi nyumbani hasa kwa kuwa njia nzuri ya kubebea mizigo. Mnyama huyu ambaye hutumiwa hasa na kina mama na watoto wa jamii ya kimasai na nyinginezo kwa ajili ya kubebea maji, kuni, majani, kupelekea mizigo sokoni na shughuli zote zile za nyumbani amekuwa hana thamani kama waliyonayo…
Chokaa au majivu huweza kuangamizi kiwavijeshi vamizi
Wakulima walio wengi katika mikoa mbalimbali hapa nchini wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiwavijeshi vamizi, mdudu ambaye husababisha hasara kubwa kwa wakulima hasa wa mahindi kwani hupoteza maelfu ya hekari za mazao endapo watavamiwa na mdudu huyu. Kuna mbinu mbalimbali za kudhibiti mdudu huyu kama vilekufanya kilimo bora mfano kupanda kwa wakati, matumizi ya mbegu kinzani (tolerant/resistant varieties), matumizi ya viumbe…
Ongeza lishe kwa kutumia njia rahisi za ufugaji samaki
Ufugaji wa samaki ni moja ya shughuli ambazo hivi karibuni imejipatia umaarufu mkubwa sana miongoni mwa wafugaji. Kazi hii imekuwa ikifanywa na makundi mbalimbali bila kujali wanafanya shughuli gani nyingine. Kutokana na uhitaji mkubwa wa lishe inayotokana na samaki, kumekuwa na aina mbalimbali za ugunduzi unaosaidia ufugaji wa samaki kwa njia rahisi. Katika makala hii tutaeleza ugunduzi mpya wa kutengeneza…
Uzalishaji wa minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki
Minyoo redworms ni chakula kizuri sana kwa kuku, bata na samaki kwani minyoo wana protini nyingi sana na kuku wakipewa au kulishia minyoo wanakua kwa haraka sana na huwafanya kuwa na maumbile makubwa sana (wanakuwa na uzito mkubwa pia). Kutengeneza minyoo ya chakula ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki. Namna ya kuzalisha Chukua mavi…
Chanjo ya matone ya mdondo; Kitaalamu I-2 vaccine
Chanjo hii ina virusi hai vya mdondo vinavyotengeneza kinga dhidi ya ugonjwa wa mdondo/kideri. Virusi hivi vimeoteshwa kwenye mayai ya kuku wasiokuwa na magonjwa anuwai. Chanjo hii inapatikana katika chupa zenye ujazo wa dozi ya kuku 100 na kuku 200. Hifadhi Chanjo ya 1-2 imehifadhiwa katika chupa za plastiki ambazo ni rahisi kusafirisha na zina mfuniko wenye sili. Ukishafungua mfuniko…






