- Mifugo

Chokaa au majivu huweza kuangamizi kiwavijeshi vamizi

Sambaza chapisho hili

Wakulima walio wengi katika mikoa mbalimbali hapa nchini wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiwavijeshi vamizi, mdudu ambaye husababisha hasara kubwa kwa wakulima hasa wa mahindi kwani hupoteza maelfu ya hekari za mazao endapo watavamiwa na mdudu huyu.

Kuna mbinu mbalimbali za kudhibiti mdudu huyu kama vilekufanya kilimo bora mfano kupanda kwa wakati, matumizi ya mbegu kinzani (tolerant/resistant varieties), matumizi ya viumbe rafiki kwa kuwaleta nchini mfano; Telenomus remus, Trichogramma. Sp na Diapetimorpha introit.

Aidha, mbinu ya kutumia chokaa (aina yeyote ya chokaa isiyokuwa na mabonge) au majivu huweza kuangamiza mdudu huyu.

Namna ya kufanya ni kuweka kiwango kidogo sana cha chokaa au majivu katikati ya shina la mhindi, na hakikisha unaweka kwenye mhindi ulioonyesha dalili ya kushambuliwa au kuvamiwa na mdudu.

Kazi ya uwekaji inaweza kufanyika wakati wa asubuhi au jioni lakini hakikisha hakutakuwa na upepo kwani chokaa ama majivu yatapeperushwa na kufanya uwekaji kukosa ufanisi.

Tindikali iliyopo kwenye majivu au chokaa ndiyo inayofanya mdudu vamizi aweze kufa na kuangamia.

Tumia majivu au chokaa kuangamiza viwavijeshi vamizi

 

 

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *