- Mifugo

Chanjo ya matone ya mdondo; Kitaalamu I-2 vaccine

Sambaza chapisho hili

Chanjo hii ina virusi hai vya mdondo vinavyotengeneza kinga dhidi ya ugonjwa wa mdondo/kideri. Virusi hivi vimeoteshwa kwenye mayai ya kuku wasiokuwa na magonjwa anuwai.

Chanjo hii inapatikana katika chupa zenye ujazo wa dozi ya kuku 100 na kuku 200.

Chanjo ya matone ya I-2 Vaccine

Hifadhi

Chanjo ya 1-2 imehifadhiwa katika chupa za plastiki ambazo ni rahisi kusafirisha na zina mfuniko wenye sili. Ukishafungua mfuniko mdomo wa chupa unatumika kudondoshea matone ya chanjo kwa urahisi na kwa usafi zaidi.

Utunzaji

Chanjo ya 1-2 inasambazwa katika hali ya majimaji. Chanjo hii ni stahimilivu kwa joto, ikihifadhiwa kama inavyoelezwa hapo kwa njia zifuatavyo;

Chanjo ndani ya jokofu kamwe isiwekwe kwenye sehemu ya kugandishia barafu (freezer), Kama hakuna jokofu, chanjo hii itunzwe kivulini, kwenye hali ya ubaridi na kutumiwa haraka iwezekanavyo.

Hifadhi ya chanjo na muda wa matumizi

Chanjo ihifadhiwe kwenye nyuzi joto kati ya 2-8 (jokofu) muda usiozidi miezi mine, nyuzi joto kati ya 25-30 muda usiozidi siku 7 na nyuzi joto zaidi ya 30 kwa siku 2. Chanjo iliyofunguliwa itumike ndani ya siku 2.

Usafirishaji

Chanjo isafirishwe kwenye hali ya ubaridi ndani ya kasha la barafu lenye barafu, vinginevyo chanjo isafirishwe kwenye chombo baridi kama kasha la karatasi lenye magazeti na barafu au chupa za plastiki za maji ya chumvi nyingi yaliyogandishwa.

Katika hali ya vijijini, chupa yenye chanjo iviringishwe kutambaa cha pamba kilichowezeshwa maji baridi na huku isafirishwe kwenye kijikapu kidogo kilichofunikwa chenye matundu makubwa yapitishayo hewa pande zote.

Matumizi

Chanjo itumike moja kwa moja toka kwenye chupa ya chanjo bila kuchanganya na kitu chochote. Weka tone moja la chanjo kwenye jico moja la kila kuku.

Muda wa kuchanja

Kuku wa umri wowote wanaweza kupatiwa chanjo. Chanjo ifanyike kila mara baada ya miezi mitatu (3)

Kumbuka

  • Epuka kuweka chanjo kwenye joto la juu na mwanga wa jua.
  • Chanjo hii ni kwa kukinga ugonjwa wa mdondo au kideri tu.
  • Chanja kuku wenye afya tu (Epuka kuchanja kuku wagonjwa).
  • Hii ni chanjo na wala siyo tiba, hivyo isitumie kuchanja kuku wagonjwa.
  • Chanjo hii haina madhara kwa vifaranga, wala ukuaji au utagaji wa mayai.
  • Kuku hupata kinga ya kutosha dhidi ya ugonjwa wa mdondo au kideri siku 7 hadi 14 mara baada ya kuchanjwa.
  • Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu (3).
  • Dozi (tone moja kwa kuku wa umri wowote (kuanzia kifaranga wa siku moja hadi kuku mzee) au wa jinsia yeyote.
  • Kama tone halikuingia vizuri kwenye jicho, rudia kwa kuweka tone la pili.
  • Kwa maelezo zaidi muone mtaalamu wa mifugo aliye karibu na wewe kwa utaalamu.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

8 maoni juu ya “Chanjo ya matone ya mdondo; Kitaalamu I-2 vaccine

    1. Karibu sana, Ni muda mrefu toka sasa toka tumerudi mtandaoni. Wakaribishe na wengine ili waweze kujisomea taarifa mbalimbali za kilimo na ufugaji zinazopatikana kwenye tovuti yetu ya MkM

  1. Ni kwanini huwa mnashauli kwamba Mara ya kuifungua Dawa itupwe ?je siwezi hifadhi ili nine nitumie kwajili ya vifaranga wajao maybe week2 zijazo?

    1. Habari

      Chanjo nyingi zina maelekezo na muda wa matumizi, na huwa mara nyingi zikishafunguliwa hazitakiwi kukaa kwa muda zinaisha nguvu. Siyo kila dawa ni ya kutupa una zingine zikifunguliwa zinaweza kuhifadhiwa katika ubaridi wa kiwango fulani na ikadumu kwa muda mrefu kulingana na dawa yenyewe na matumizi yake na muda ila chanjo nyingi zikishafunguliwa hazitakiwi kukaa huwa zinapoteza nguvu.

      Hakikisha unafuata ushauri wa wataalamu na jinsi dawa ama chanjo ilivyoandikwa matumizi, muda na uhifadhi wake

  2. Nataka kuanza kufuga kuku wa nyama sijajua ninaanzaje kitaalam maana ninafuatilia sana kwa wanaofuga sasa nataka nijaribu au kwa kiswahili nataka niingie vitani

    1. Habari Bw. Freeman. Hongera sana kwa kupata hamasa ya kufanya ufugaji wa kuku wa nyama, karibu Mkulima Mbunifu tuko tayari kukupa kile tutakachoweza. Uliza tu nasi tutakujibu. Karibu sana

  3. Habari, Nina wazo la kumwagilia shamba langu la migomba kwa kutumia gun sprinkler, ila chanzo changu cha maji ni kisima kilichokuwa drilled, i m just thinking, nikitumia tank la l4000 itawezekana?kwasababu nahitaji kutumia pressure pump! isije ikafia wakati na-pump maji tu all day.

    1. Habari Bw. Seiph

      Hongera sana kwa mawazo chanya na kwa kilimo cha migomba lakini kulingana na aina ya kilimo unachohitaji kukifanya sidhani kama guna sprinkler inafaa kumwagilia zao hili kwani maji yanatoka kwa juu sana na kwa kusambaa na kumbuka migomba ina majani yanayofunga na mapana hivyo maji mengi yatapotea angani kwenye majani na hayatashuka chini ardhini. Gun sprinkler inafaa kwa kilimo cha mazao ya bustanini kama vile mbogamboga, viazi nk.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *