- Mifugo

Ufugaji holela wa kuku haufai na ni hatari

Sambaza chapisho hili

Nimekuwa mfugaji wa kuku kwa kipindi cha miaka mingi sana, tatizo ni kwamba kuku wangu hawana banda maalumu na hukutana nao jioni tu wanapoingia jikoni, na kutoka asubuhi, nimesoma kidogo kwa jirani yangu aliekuwa na Mkulima mbunifu juu ya ufugaji wenye tija, je nikianza haitanigharimu sana kwa kuwa wao hujitafutia chakula wenyewe?-Haule, Iringa.

Kuku kama ilivyo kwa mifugo wengine, wanahitaji kuwa na banda lao, na kupatiwa matunzo stahiki. Kwa kufanya hivyo, utaweza kufahamu maendeleo ya mifugo yako na pia kujipatia faida kadhaa zinazotokana na ufugaji wenye tija.

Moja ya faida hizo ni pamoja mbole, mayai, na idadi ya kuku wako kuongezeka.

Ni hatari sana unapofuga kuku wako kiholela kwani hupotea ovyo kwa kuliwa na wanyama porini, wezi, kutagia porini sehemu ambayo huwezi kupata mayai kwa ajili ya chakula na hata kuuza, pamoja na kufa kutokana na magonjwa ya aina mbalimbali.

Kwa hakika kulingana na mazingira uliyopo kuku wa kienyeji hawana gharama kubwa sana kuwatunza kwani hula vyakula vya kawaida tu vinavyopatikana katika mazingira ya mkulima.

Unaweza kutumia pumba zinazotokana na mahindi ambayo pengine yamekobolewa kwa ajili ya matumizi ya familia na ukajipatia chakula cha kuku. Mabaki ya jikoni, na majani laini kutoka shambani mwako. Hakika hii si gharama kubwa.

Ni vizuri pia ukawekeza kidogo kuwatengenezea au kuwanunulia chakula ambacho kina virutubisho ili kuweza kupata faida zaidi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *