- Kilimo

Matumizi ya Molasi na faida zake kwa uzalishaji wa mazao

Sambaza chapisho hili

Katika kilimo, matumizi ya Molasi ni muhimu kwa kuboresha hali ya udongo, kudhibiti wadudu, kuwezesha udongo kuwa na rutuba, kurekebisha hali ya udongo na pia kupunguza matatizo kwa mimea inayopandikizwa.

Matumizi ya Molasi husaidia kusafisha mipira ya umwagiliaji lakini pia utafiti unaonyesha kuwa Molasi husaidia kuboresha ubora wa udongo.

 

Matumizi na kiasi cha kutumia

  1. Kuboresha umbile la udongo. Molasi husaidia kuboresha udongo na kuunganisha chembe za udongo na chembe za rutuba na viumbe hai ardhini. Ili kuwa na matokeo mazuri, Molasi ichanganywe kwenye udongo mfululizo kwa kiasi cha lita 20-25 kwa hekta kwa wiki na kipindi chote cha kumwagilia.
  2. Kuongeza viumbe hai kwenye udongo. Kwa ajili ya umajimaji wake, molasi inaweza kuchanganywa kwenye maji kwa urahisi. Ingawa inafanya kazi kwa muda mfupi, lakini inasababisha kuongeza uhai wa udongo. Matumizi endelevu ya molasi inaongeza viumbe hai kwa asilimia 0.5-1 kwa mwaka.
  3. Inasaidia kupunguza athari za wadudu kwenye udongo (nematodes) iwapo itatumika kwa muda wote wa uzalishaji. Tumia lita 20-25 kwa kiwango katika hekta moja.
  4. Molasi pia husaidia kwenye maeneo yenye tatizo la mchwa na wadudu wanaosafirishwa na mchwa. Kiasi cha kutumia ni kilekile cha lita 20-25 kwa hekta kwa wiki na itumike wakati wote wa kumwagilia.
  5. Kwa kutumia molases ina asili ya tindikali, inafanya kazi ya kusafisha mipira ya umwagiliaji, mchanganyiko wa lita 25 za molases katika kubiki mita 10 za maji.
  6. Kuna dalili kuwa molasi inasaidia mizizi kuwa na nguvu ya kufyonza virutubisho katika udongo hasa mizizi inapokuwa imekosa maji.

Matumizi ya molasi ni muhimu kwa sababu inafanya kazi ikiwa hai sio sawa na kemikali, na kwa sababu udongo unahitaji ili kuwezesha ukuaji wa mizizi ya mimea, kwa kuweka uwiano wa viumbe hai katika udongo na kuboresha muundo wa udongo unaoruhusu maji kusafiri bila shida.

Mizizi yenye afya huwezesha mmea kufyonza virutubisho ardhini na mmea kuwa na afya. Umbile na udongo wenye virutubisho ndio msingi wa uzalishaji bora wa mazao ya mboga na matunda.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *