- Binadamu

Ubuyu na faida zake katika mwili wa binadamu

Sambaza chapisho hili

Ubuyu ni tunda ambalo hupatika­na kwenye miti jamii ya Adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbali-mbali wengi tukiutumia kama ma­tunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia kuongeza ladha kwenye vyakula.

Ubuyu umekuwa tunda lenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu. Ni tunda la asili na linapatikana porini hasa katika kanda kame (semi-arid). Vitu vyote vilivyomo kwenye ubuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Faida za ubuyu

Ubuyu una uwezo mkubwa wa kui­marisha kinga ya mwili, kuimarisha mifupa, kusaidia mfumo wa umeng’e-nyaji chakula kupunguza maumivu, uvimbe na kusisimua utengenezaji wa seli na tishu mpya. Pia, husaidia kupu-nguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa sugu.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine

  • Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
  • Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kalisiamu (Calci­um) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu a-mbayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
  • Husaidia kujenga neva za faha­mu mwilini.
  • Virutubisho vya kulinda mwili
  • Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambazo ni muhimu katika kuo-ndoa sumu mwilini na ume-ng’enyaji wa madini ya chu­ma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili wa binadamu huwa pia na vitamin B2.
  • Unaongeza kinga ya mwili sa­babu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
  • Huongeza nuru ya macho
  • Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
  • Ina maginesiamu ambayo husai-dia kujenga mifupa na meno
  • Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Juice ya ubuyu

Juisi ya ubuyu ni moja kati ya juisi zilizopata wanywaji wengi duniani kote katika miaka ya hivi karibuni, Juisi ya ubuyu ina virutubisho vya kalsiamu (Calcium) na madini ya chu­ma (Iron) ambavyo ni muhimu katika miili yetu hasa kwa watoto, wajawazi­to na wazee.

Jinsi ya kuandaa juice ya Ubuyu

  • Katika kuandaa juisi ya ubuyu unahitajika kuwa na unga wa ubuyu au ubuyu wa mbegu, maji safi, sufuria, kijiko au mwiko, sukari, chujio, jagi na jiko.
  • Ubuyu wa unga;changanya vi­kombe 6 na maji vikombe 9.
  • Ubuyu wa mbegu; changanya vikombe 3 na maji vikombe 12.
  • Weka sukari kiasi unachotaka, changanya vizuri na mwiko ki­sha bandika jikoni acha iche-mke kwa kiasi cha kutosha ili kuuwa vijidudu vya magonjwa kama vitakuwemo na itakuwa tayari kwa matumizi.
  • Acha ipoe, alafu koroga na uweke katika jagi tayari kwa kunywa.

Matumizi

Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

NGALIZO: Ili upate faida za juisi ya ubuyu, kama inavyoelezwa hapa, lazima upate ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *