- Kuku, Mifugo

Fahamu mikakati rahisi inayoweza kutumika ili kupanua mradi wa ufugaji wa kuku

Sambaza chapisho hili

Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga.

Kuku ni ndege maarufu na ana-yefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii.

Kwa nini ni vigumu kuongeza kipa­to kutokana na ndege huyu mwenye umaarufu mkubwa na bidhaa zake zinathaminiwa na kuhitajika?

Kuna wakati mfugaji anajikuta ka­tika wakati mgumu akiwa na uhitaji wa haraka wa pesa, kuku ndiye mfu­go wa kwanza kuuzwa.

Wakati mwingine, mgeni muhimu akifika kutembelea familia, mara nyingi kama kuku wapo, huchinjwa na kufanywa kitoweo. Hivyo, idadi ya kuku kwa mfugaji inapungua au kuko­sa kuongezeka.

Hii inakuwa changamoto katika kukuza ufugaji wa kuku na kufanya bi­ashara yenye tija na kusababisha ku­kata tamaa. Katika hali kama hii hasa vijijini, inakuwa vigumu kwa mfugaji kutoka kwenye hali ya umaskini.

Fursa katika ufugaji wa kuku

Kuna fursa ya kutoka kwenye uzalisha­ji mdogo na kwenda hatu kwa hatua kufikia uzalishaji mkubwa, ambao unaleta pato kubwa na kuhakikisha usalama wa chakula na kujitosheleza kwa chakula. Hii inaweza kufanikiwa ikiwa wafugaji wadogo wa kuku wata-panua viwango na idadi ya mifugo yao.

Ongeza idadi ya kuku

Unahitaji kuongeza idadi ya kuku ili iwe na maana kibiashara. Gharama ya kuwatunza kuku inashuka idadi yao inapopanda.

Chagua na kuwatenga kuku wenye hali nzuri wa mbegu, kulalia na kuto­toa mayai. Usiuze kundi hili la kuku, badilisha tu jogoo. Wakizeeka au uwezo wao wa kutaga ukishuka, una-wauza au kuwabadilisha. Hii inatoa uhakika wa kuwa na mayai ya kuto­sha kila wakati, na vifaranga wapya kila wakati.

Mara nyingi, wafugaji ambao wa­naanza huwa wanatilia mkazo sana makazi ya kuku. Wanajenga nyumba za gharama kubwa, mwishowe, ha­wana pesa za kununua kuku kuanza ufugaji, au wananunua na kushindwa kuwatunza.

Unapoanza zingatia kuongezeka kwa idadi, sio kwenye nyumba za gharama kubwa. Unaboresha makazi pole pole unapojenga kulingana na idadi ya kuku.

Ikiwa una nafasi, unaweza kuwe­ka ua na kutenga sehemu ya kuku kutembea wakati wa mchana. Hii inawapa nafasi ya kula vyakula vyenye kijani kibichi (vitamini) na wadu­du (protini), changarawe (nzuri kwa mmeng’enyo wa chakula), na kinyesi chao kinarutubisha udongo. Baadaye, wanarudi kwenye makazi yao amba­po wanapata chakula cha nyongeza kilichotengenezwa nyumbani au kili­chonunuliwa madukani.

Chakula kinachozalishwa shamba­ni kinapendekezwa kwa kuku wa asili. Inaweza kuwa mchanganyiko wa na­faka ya mahindi

Kuku hushambuliwa na magonjwa na husababisha hasara kubwa katika ufugaji wa kuku. Ugonjwa wa kutisha zaidi ni Kideri/Mdondo (Newcastle). Punguza uwezakano wa maambuzi ya magonjwa kwa kuwapa kuku lishe bora, weka makazi safi, na kufuata utaratibu wa chanjo. Pia, wape kuku dawa ya miyoo, la sivyo, chakula una-chowapa kitakuwa cha kulisha vime­lea.

Ikiwa mfumo wa ufugaji huria, wape dawa ya minyoo kila baada ya mwezi moja, na katika mfumo wa nusu huria au ndani wape dawa ya minyoo kila baada ya wiki 6-8. Pia, nyunyiza majivu au chokaa au dawa za kuua wadudu kila mara unapofanya usafi wa banda.

Tenga kuku wapya kutoka nje ya shamba lako kwa angalau wiki mbili. Kwa njia hii, unalinda kuku wako dhi­di ya vimelea ambavyo vinaweza kuletwa kutoka shamba lingine.

ANGALIZO: Kukizuka maambukizi ya magonjwa, ondoa na kuchoma au kuzika kuku wote waliokufa.

Kuwa na daktari wa mifugo karibu kwa ajili ya ushauri kila wakati una-poona dalili au kushuku kuku wako ni wagonjwa.

Ungana na wafugaji wengine

Pengo moja kubwa katika kukuza sekta ndogo ya kuku nchini ni kutokuwa na vikundi, mashirika na majukwaa ya wafugaji kuku. Mashirika ya wakulima yaliyopo yameundwa vibaya, viongozi ambao hawana maono na uzoefu wa kibishara, na uwezo wa kujenga na kudumisha makundi ya wafugaji.

Ungana na wafugaji wengine ili kuweka mifumo thabiti ya kuzalisha kuku wa hali ya juu. Hii itawawezesha kufikia soko la mbali, kununua chaku­la cha kuku kwa wingi na kwa bei ya jumla. Mnaweza kutengeneza chaku­la cha kuku, na kununua malighafi kwa bei ya chini. Pia, kuna nafasi ya biashara ya kuuza chakula cha kuku mlichotengeneza au malighafi kwa wafugaji wengine katika eneo lako na kwingineko. Hii itaongeza njia za ki­kundi kupata faida.

Wekeza faida

Usiuze kuku mmoja mmoja. Uza kuku wengi mara moja ili upate pesa ya kufanya jambo la maana. Uza wakati bei katika soko iko juu kabisa. Fuatilia soko la kuku ili kujua mfumuko wa bei. Hii itakuwezesha kuepuka hasara. Jambo la muhimu ni kuwekeza sehemu ya faida kwa kuongeza idadi ya kuku, kuboresha malisho, makazi na dawa za chanjo, na matibabu ikiwa magonjwa yatazuka.

Unaweza kutumia mapato kuto­kana na mauzo ya mayai ili kulipa gharama za kila siku za kuendesha ufugaji, na pesa kutoka kwa mauzo ya kuku kupanua biashara yako ya kuku. Hakikisha tu, hauli kuku anayetaga yai. Ukifanya hivyo, utakuwa unazika biashara yako.

Chukua hatua

Je, wewe ni mfugaji wa kuku? Ni mi­kakati gani unatumia kupanua ufugaji wako na kuongeza mapato? Wasili­ana nasi ili tuwashirikishe wafugaji wengine uzoefu wako.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *