Kumekua na maswali kadhaa juu ya kuanzisha kilimo hai. Yamkini, wewe pia unajiuliza swali hili, vile unavyoweza kuzalisha kwa mfumo wa kilimo hai shambani mwako. Jarida la Mkulima Mbunifu ni mahususi kwa ajili yako na katika makala hii tunakukumbusha tena. Kama una nia thabiti ya kuanzisha kilimo hai, fuata hatua zifuatazo; Angalia uwezekano wa kupata soko kwanza Jiulize mwenyewe: Ni…
Mifugo
Changamoto katika kilimo na ufugaji msimu wa mvua
Kilimo katika msimu wa mvua Huu ni msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini. Bila shaka wengi wetu ni wakulima na wafugaji hivyo bado tunaendelea na shughuli zetu za kila siku. Je, ni changamoto zipi unazopitia katika msimu huu wa mvua kwenye shughuli zako za kila siku za kilimo? Tushirikishe/tueleze ili tuweze kupeana ushauri nini chakufanya Tuma ujumbe wako hapa…
Ufugaji wa samaki kibiashara ni njia rahisi yakuongeza kipato
Kumekuwa na mfumko wa watu wengi mijini na vijijini kuingia katika ufugaji wa samaki. Miradi hii huwagharimu fedha nyingi, lakini hufa baada ya muda mfupi. Ili mfugaji aweze kuwa na ufugaji wenye tija, hana budi kujifunza ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vifaa vingine vinavofanana na hivyo, vyenye uwezo wa…
Tahadhari za kuchukua nyakati za msimu wa mvua katika ufugaji samaki
Ufugaji wa samaki una kanuni na taratibu za kufuata ili kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa. Msimu wa masika ni muhimu kuufuatilia ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. Katika makala hii Mkulima Mbunifu linakuangazia hatua muhimu za kuzingatia wakati wa masika ili kufanya ufugaji samaki wenye tija. Nyakati za msimu wa mvua ni vema kuzingatia hatua zifuatazo ili kuepuka madhara…
Fahamu mikakati rahisi inayoweza kutumika ili kupanua mradi wa ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni ndege maarufu na anayefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Kwa nini ni vigumu kuongeza kipato…
Ulishaji wa majani makavu: Usisahau maji
Kabla ya kulisha wanyama majani makavu ni muhimu sana kufahamu ni kwa namna gani yanahitajika kulisha kwani majani haya ni tofauti na majani mabichi. Kiwango cha majani makavu kiwe kidogo zaidi ya majani mabichi. Robota moja la kilo 15 la majani makavu ni sawa na kilo 75 za majani mabichi, na yanaweza kulishwa kwa ng’ombe anaetoa maziwa vizuri mara moja…
Fuata kanuni sahihi za kilimo upate mavuno bora
Wakulima walio wengi wamekuwa wakijikita zaidi katika matumizi ya mbolea ili kupata matokeo mazuri katika kilimo, na kusahau kuwa kanuni bora za uzalishaji pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka na kupatikana kwa mavuno yenye ubora. Nini cha kuzingatia ili kupata mavuno bora Ni lazima mkulima kufuata utaratibu wa uzalishaji wa mazao katika kila msimu wa kilimo. Hatua zifuatazo ni lazima…
Njia bora ya utunzaji wa ng’ombe wa maziwa
Nina mradi mdogo wa ng’ombe wa maziwa, ninahitaji kuboresha, naomba ushauri namna ya kuwa na banda bora na matunzo yake kwa ajili ya ng’ombe wangu Ng’ombe wa maziwa wanaweza kuzalisha vizuri kutokana na kuwa na mazingira mazuri, banda zuri na lishe. Zingatia usafi na uhakikishe kuwa ng’ombe wana nafasi ya kutosha. Nafasi: Kila ng’ombe mkubwa anahitaji walau skwea mita 8,…
Zalisha matunda kwa malengo
Moja ya mazao ambayo wakulimwa wamekuwa wakizalisha kwa ufanisi mkubwa na kupata mavuno mazuri, ni matunda ya aina mbalimbali. Ambapo kulingana na mazingira waliyopo, wakulima wamekuwa wakizalisha aina mbalimbali na kwa misimu tofauti. Pamoja na mafanikio hayo, wakulima wamekuwa wakizalisha aina hizo za matunda bila kuwa na malengo kamili kuwa ni nini wanachohitaji kutokana na matunda hayo, jambo ambalo mwisho…
Kuku chotara wanahitaji chanjo kwa utaratibu maalumu
Ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara ni ufugaji ambao hujumuisha muunganiko au mchanganyiko wa aina mbili tofauti za kuku. Kuku chotara wana faida nyingi sana kwa mkulima ikiwa ni pamoja na ustahimilivu wa magonjwa hivyo kupunguza gharama za kutibu. Utagaji mkubwa wa mayai mengi mpaka kufikia 240 kwa mwaka kama ukiwalisha vizuri endapo watalishwa vizuri. Halikadhalika, kuku hawa wanakua haraka…