- Mifugo

Ufugaji wa mbuzi hutegemea lishe sahihi

Sambaza chapisho hili

Ufugaji wa mbuzi ni moja ya miradi ya ufugaji rahisi lakini yenye changamoto nyingi ikiwa mfugaji hatazingatia maswala muhimu yanayohitajika kufuatwa kwa usahihi katika mradi huu hasa juu ya lishe.

Kama mfugaji makini, hakikisha unafahamu namna na nini cha kulisha mbuzi ili uweze kufanya ufugaji wenye tija na utakaokupatia kipato sahihi kulingana na uzalishaji unaofanya.

Baadhi ya vidokezo muhimu

  • Kwa asili mbuzi ni watafutaji binafsi wazuri wa malisho. Mbinu bora ya ulishaji wa mbuzi ni kuhakikisha wanapata malisho mazuri kwasababu afya na ukuaji wa mbuzi hudorora kwa ufugaji wa ndani.
  • Mbuzi wanapaswa kulishwa mara tatu kila siku, na maji yakipatikana wakati wote.
  • Mbuzi wenye afya dhaifu wanapaswa kutengwa na wale wenye afya imara.
  • Baada ya kuzaliwa tu, watoto wa mbuzi wanapaswa kunyonya maziwa ya mama kwa takribani muda wa dakika 20 mpaka 30.
  • Maziwa huwa na harufu mbaya kama mbuzi atalishwa kwenye malisho yenye harufu au kama mbuzi jike hutunzwa pamoja na mabeberu.

Lishe ya mbuzi

Mbuzi wanaolishwa vizuri huzalisha maziwa na nyama zaidi. Mbuzi jike katika mwezi wa mwisho kabla ya kuzaa anahitaji protini na vyakula vyenye nguvu zaidi ya mbuzi wa kawaida.

Maji

  • Mbuzi wa maziwa wanahitaji angalau lita 3-8 za maji masafi katika kipindi sahihi.
  • Mbuzi wanaokula malisho makavu huhitaji zaidi maji
    kupata nguvu.
  • Vyakula vya nishati kama vile mizizi, ndizi, molasi, matunda, na keki ya mafuta huhakikisha kwamba mbuzi wapo hai muda wote.
  • Soya, pamba, alizeti, karanga na nazi hutoa nguvu mara 2 – 3 zaidi ya vyakula vya wanga kama majani na matawi ya miti.

Protini

  • Mbuzi huhitaji protini zaidi kuliko ile waipatayo katika malisho.
  • Majani ya kijani, njegere na maganda ya mgunga, soya, pamba, njugu, na majani kutoka leucaena, sesbania, na gliciridia ni vyanzo vizuri vya protini.
  • Takataka za kuku ni chanzo kingine kizuri cha protini.

Madini

  • Mbuzi wanahitaji kalsiamu, sodiamu, fosforasi, chuma, shaba na aiyodini.
  • Kijani cha majani ya miti, vichaka, na mbegu ya nafaka ni vyanzo vizuri vya fosforasi na kalsiamu.
  • Majani yenye weusi ni vyanzo vizuri vya madini ya chuma.
  • Mbuzi wenye ukosefu wa madini ya aiyodini wanaweza kuzaa watoto dhaifu, walioharibika na njiti.

Vitamini

  • Mbuzi wenye upungufu wa vitamini A hukabiliwa na matatizo ya macho, maambukizo ya ngozi na matatizo ya kupumua na shida katika mimeng’enyo ya chakula.
  • Mbuzi wenye upungufu wa vitamin huzaa watoto dhaifu.
  • Pale mbuzi wanapokuwa katika malisho, hupata vitamini mbalimbali kutoka katika mimea wanayo kula.
  • Viazi vitamu hutoa zaidi vitamini A na majani ya viazi hivyo vitamu hutoa vitamini C.

Kulisha mbuzi kwa ajili ya soko la nyama

  • Miezi mitatu baada ya kuachishwa, mbuzi watoto wanapaswa kuwa na uzito wa kilo 15, kutegemea na aina ya mbuzi na mfumo wa ulishaji.
  • Beberu kwa ajili ya soko la nyama wanaweza kuhasiwa kutoka wiki mbili mpaka miezi miwili ya umri ili kupata zaidi uzito.
  • Beberu hulishwa mara mbili kwa siku na nusu kilo ya protini kuongeza uzito wao na kupata mapato zaidi katika masoko ya nyama.
  • Kutoka miezi 6-12, mbuzi wa nyama wanapaswa kulishwa zaidi majani ikiwa ni pamoja na mabua ya kijani ya mahindi na nyasi ya jamii kunde.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *