Nyanya chungu (ngogwe) Chagua sehemu ya kufanyia kazi Chagua ngogwe zilizokomaa vizuri Osha ngogwe kwa maji safi Kata vipande kwa wima (Vertically) Kata vipande vyembamba vyenye unene wa milimita 2-3 Tumbukiza vipande vilivyokatwa ndani ya juice ya maji ya limao ili kutunza rangi yake ya asili. Panga katika matrei tayari kwa kukausha Kausha kwa muda wa siku tatu hadi ifikie…
Usindikaji
Sindika karoti na nazi kupata mafuta na kukuza pato
Vijana wengi kwasasa wameanza kuthamini na kuwa na mwamko katika ujasiriamali kutokana na uhaba wa ajira lakini pia uhitaji mkubwa kwa walaji wa bidhaa salama zinazozalishwa ndani ya nchi. Wengi wao wamejikita kusindika mazao mbalimbali na kupata bidhaa bora zinazowasaidia kupata kipato kwa urahisi. Bi. Christina Macha ni miongoni mwa wasindikaji wa mafuta yanayotokana na mazao mbalimbali kama vile nazi,…
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Unaweza kusindika stroberi kwa kutengeneza jamu
Wakulima wengi wamekuwa na mawazo finyu hasa katika kutatua changamoto zitokanazo na upotevu wa mazao yao shambani jambo lililowapelekea, kusahau kuwa kuna mbinu mbalimbali zakukabili changamoto hizi kama vile kujikita katika utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na mazao. Katika nakala hii Mkulima Mbunifu inakuangazia kijana Charles Watson kutoka Mbeya aliyejikita katika kilimo cha stroberi na uchakataji wa bidhaa zitokanazo na zao…
Jifunze njia rahisi ya kukausha viazi vitamu
Viazi vitamu ni moja ya mazao ya mizizi ambayo huvumilia ukame. Zao hili hulimwa karibu katika mikoa yote. vitamu hasa vya rangi ya karoti vina virutubishi vya vitamini A kwa wingi ambavyo vinahitajika sana katika mwili. Kulingana na uzalishaji mwingi ni muhimu kukausha viazi vitamu ili kuviongezea thamani, ubora na matumizi yake. Viazi vitamu husindikwa pia ili kupata viazi vilivyokaushwa,…
Namna ya kusindika korosho mara baada ya kuvuna
Korosho ni zao lenye matumizi mengi sana, lakini kubwa kuliko yote ni kwamba kuliwa kama kitafunwa (snacks) wakati wa kunywa chai, juisi, maziwa au kahawa. Makala hii inakusudia kutoa mafunzo ya namna ya kuandaa korosho kwa matumizi ya nyumbani. Hii itawasaidia wakulima wapya wa mikoa hasa iliyoingia kwenye uzalishaji wa zao hili kwa mara ya kwanza. Jinsi ya kuandaa korosho…
Sindika maziwa kuongeza pato na uepuke hasara
Kabla ya kusindika maziwa ya mgando au mabichi ni lazima kufanya vipimo vya awali ili kujua kama maziwa yanafaa kusindika au hayafai. Kipimo kikubwa kinachotumika kupima maziwa ni alkoholi (Ethanol) Kipimo hiki hutumika kutambua maziwa yaliyoharibika na maziwa yaliyoanza kuganda. Namna ya kupima Chukua kiwango kinacholingana cha Alkoholi (ethanol) na maziwa mabichi kisha changanya pamoja kwa kuweka katika chombo maalum…
Unaweza kusindika ngozi kiasili kupata bidhaa bora
Usindikaji wa viwandani unahitaji mitambo mikubwa, maeneo makubwa nguvu kazi kubwa, malighafi nyingi. Hivyo inahitaji mtaji mkubwa. Njia hii pia inahitaji kemikali za viwandani hivyo sio rafiki kwa mazingira. Usindikaji wa asili ni rahisi kwani malighafi za uchakataji hupatikana katika mazingira yanayotuzunguka. Njia hii inashauriwa sana kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana mitaji mikubwa na unaweza kuchakata ngozi moja kwa…
Usindikaji wa Mvinyo kwa matunda ya asili
Vijana wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kusindika mazao kutumia malighafi za hapa nchini. Mvinyo ni neno linalotokana na neno la kireno vinho, ni kinywaji kinacho tengenezwa kutokana na majimaji ya matunda mbalimbali. Kuna aina nyingi za mvinyo kufuatana na matunda yaliotumika. Katika Makala hii Mkulima Mbunifu inaangazia Kijana wa kike kutoka mkoani Mbeya alivyoamua kujitoa kimasomaso katika kusindika matunda kupata mvinyo…