- Usindikaji

Usindikaji wa mbogamboga na matunda

Sambaza chapisho hili

Nyanya chungu (ngogwe)

  • Chagua sehemu ya kufanyia kazi
  • Chagua ngogwe zilizokomaa vizuri
  • Osha ngogwe kwa maji safi
  • Kata vipande kwa wima (Vertically)
  • Kata vipande vyembamba vyenye unene wa milimita 2-3
  • Tumbukiza vipande vilivyokatwa ndani ya juice ya maji ya limao ili kutunza rangi yake ya asili.
  • Panga katika matrei tayari kwa ku­kausha
  • Kausha kwa muda wa siku tatu hadi ifikie kuwa kama ngozi.

Mbogamboga jamii ya majani

Majani ya maboga na mchicha

  • Chagua majani mabichi na laini
  • Chambua mboga na kuondoa nyuzinyuzi
  • Osha majani yako kwa maji safi
  • Tumbukiza mboga kwenye maji ya vuguvugu kwa dakika 3-5 ,kisha weka mboga kwenye maji ya baridi Kwa dakika 1 ipoe ili kuzuia kue-ndele kuiva zaidi
  • Toa na iache mboga ichuje maji
  • Weka katika matrei tayari kwa ku­kausha
  • Kausha mboga ikauke vizuri kwa muda wa siku 3 (pia itategemea hali ya hewa husika)

Viazi vitamu

  • Chagua viazi bora (smooth and firm), osha vizuri kwa maji safi
  • Vukiza viazi kwenye maji ya moto hadi viwe laini (30-40) dk
  • Vimenye viazi vyako
  • Katakata vipande vyenye ukubwa wa (3-5) mm.
  • Panga katika matrei tayari kwa ku­kausha.
  • Kausha mpaka kufikia hatua yaku­vunjika.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *