- Kilimo, Usindikaji

Jifunze kusindika bamia

Sambaza chapisho hili

Bamia ni aina ya tunda mboga lenye utajiri wa virutubishi ambavyo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu hasa katika usagaji wa chakula.

Faida za ulaji wa bamia

  • Umeng’enyaji na uwekaji sawa wa mfumo wa sukari mwilini.
  • Kulainisha choo na kuzuia kuvimbiwa.
  • Kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili.
  • Kuwepo kwa wingi wa virutubisho vya protini ambavyo vinahitajika katika mwili wa mwanadamu.
  • Wingi wa virutubisho vya vitamin A na B.
  • Husaidia kuzuia kuzaliwa kwa mtoto mwenye tatizo la kupasuka kwa uti wa mgongo au kuwa na tatizo la mgongo wazi.
  • Husaidia kuongeza kinga ya mwili.
  • Kudhibiti matatizo ya vidonda vya tumbo.
  • Husaidia kuzuia saratani ya tumbo.

Namna ya kusindika bamia

  • Chuma matunda kisha yaoshe kwa maji safi na salama.
  • Mara baada ya kutoa kwenye maji, anika kwa muda kidogo kuhakikisha maji yamekauka, yaani usikate bamia zikiwa bado zina maji.
  • Mara baada ya kukausha, kata vipande vidogo-vidogo na vyembamba.
  • Panga vipande hivyo kwenye kaushio la jua moja moja bila kuweka kipande juu ya kingine.
  • Acha bamia zikauke kiasi cha kuweza kufaa kusaga.
  • Saga bamia kisha hifadhi unga kwenye mifuko maalumu ya kuhifadhia tayari kwa matumizi au kupeleka sokoni.
  • Unga huu ukihifadhiwa vizuri huweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila kuharibika.

Namna ya kutumia unga huu

Unga wa bamia hutumika kwa kutengeneza juisi, yaani kukoroga unga huu kwenye maji au kwa kuchanganya na matunda mengine.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *