Homa ya nguruwe ni ugonjwa hatari wa nguruwe unaosababishwa na virusi aina ya African Swine Fever vinavyoshambulia na kuharibu mfumo wa damu. Virusi vinavyosababisha homa ya nguruwe haviambukizi binadamu. Virusi vinavyosababisha homa ya nguruwe huishi kwenye miili ya ngiri bila kusababisha ugonjwa Kupe laini walioko katika mashimo wanamoishi ngiri, hupata virusi vya homa ya nguruwe wanaponyonya damu kutoka kwa ngiri…
Mifugo
Makosa wanayofanya wafugaji wa nyuki wadogo na jinsi ya kukabiliana nayo
Nyuki ni wadudu wadogo lakini ni wadudu wenye uwezo wa kutengeneza mazao ya chakula na biashara kama asali na nta. Ufugaji wa nyuki pamoja na kumpatia mfugaji pato lakini pia nyuki husaidia katika kuhifadhi mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Baadhi ya wafugaji wa nyuki huwa na matamanio ya kupata faida kubwa kutokana na kazi hii lakini…
Maswali toka kwa wasomaji wa Mkulima Mbunifu kwa njia ya simu
Ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu, ni furaha yetu kuwa umeendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali zinazochapishwa kwenye jarida hili. Pia tunashukuru wewe uliefatilia na kutaka kufahamu kwa undani kwa kuuliza maswali pale ambapo hujaelewa ama umekwama. Pia tunashukuru kwa mchango wako katika kutekeleza kilimo hai. Katika makala hii ni baadhi tu ya maswali yaliyoulizwa na wakulima wasomaji wa…
Tushirikiane kupata soko la mazao ya kilimo hai
Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai. Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwenda, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali…
Unaweza kuokoa pesa nyingi kwa kutumia mwarobaini
Mimi ni msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu, na nimefaidika mengi sana. Ningependa kufahamu kuhusiana na mti wa mwarobaini ambao nimekuwa nikisikia kwa muda mrefu kuwa unatibu wanyama na binadamu. Je naweza kuutumia kutibu kuku na mifugo mingine ninayofuga, na je unafaa kwa mazao? Msomaji MkM Mwarobaini () ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali.…
Njia bora ya kugawanya makundi ya nyuki wadogo
Nyuki wasiong’ata maarufu kama nyuki wadogo hufikia kiwango cha kuwa kundi kubwa lenye kuhitaji kuendelezwa kutoka katika mzinga mama na kuelekea katika mzinga mpya. Zoezi la kugawanya makundi ya nyuki huhitaji utalaamu na uangalifu wa kutosha ili kusaidia ugawanyaji wa kundi kuwa wenye tija kwa mfugaji. Kuna faida kubwa ya kugawanya makundi ya nyuki wasiong’ata Huongeza idadi ya nyuki katika…
Tumia mpungate/kakati kutibu ugonjwa wa ndigana baridi
Ng’ombe wangu anapata choo kigumu sana na mara nyingine, kinaambatana na ute kama makamasi na damu, huu ni ugonjwa gani, na nasikia kuna dawa za kienyeji zinazotibu! Ni dawa gani, na inaandaliwaje? Kuna uwezekano mkubwa kuwa ng’ombe wako anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama ndigana baridi au kitaalamu Anaplasmosis. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria ambapo mnyama hujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na…
Kuroila: Kuku wa ajabu wenye faida kubwa
Kuroila wanaweza kufugwa ndani na kulishwa katika banda au kuachiwa huru kujitafutia. Wanaweza kulishwa kwa kutumia mabaki ya vyakula au vyakula maalumu. Kuroila ni aina ya kuku wa kienyeji ambao wanakuwa kwa haraka sana na hutaga mayai mengi zaidi ukilinganisha na aina nyingine ya kuku, wawe wa kienyeji au wa kisasa. Kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki, kuku…
Re-Thinking Food: Transforming Food Systems for People and Planet | Frank Eyhorn | TEDxIHEID
Just click here to watch Climate change, biodiversity loss, poverty, health issues: what we eat and how we produce our food is shaping the face of our planet and of our societies like no other human activity. The hidden costs of cheap food are mind-blowing. At the same time, food is currently one of the most powerful levers for changing…
Msimu huu wa mvua otesha matete, lishe muhimu kwa ufugaji wa ng’ombe
Majani ya matete ni moja ya zao maarufu kwa lishe ya mifugo Afrika mashariki. Hata hivyo, wafugaji wengi wamekuwa wakilipuuzia huku wakikosesha huduma muhimu zinazohitajika kwa ajili ya uzalishaji mzuri. Moja ya tatizo kubwa katika uzalishaji wa maziwa ni kukosekana kwa malisho sahihi na ya kutosha kwa ajili ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na kipato, hasa wakati wa…