- Kilimo, Mifugo

Jinsi ya kushirikiana na Mkulima Mbunifu

Sambaza chapisho hili

Sasa unaweza kushirikiana na jarida la MkM kutoa mafunzo na habari kwa wakulima kuhusu mbinu na teknolojia tofauti zinazowezesha kuboresha uzalishaji na kuleta faida kwa mkulima na jamii kwa ujumla.

Hii ni fursa ya kuwekeza zaidi katika kufikisha matokeo ya utafiti na ubunifu unaowanufaisha wakulima kwa wakulima wenyewe.  Kuna tafiti nyingi tu lakini njia za kusambaza kwa wakulima ni chache na haziwafikii wakulima wote, lakini tukifanya kazi kwa ushirikiano tutaweza kuwafikia wengi.  Baadhi ya mikakati ya kujenga ushirikiano huu ni;

  • Kuchangia makala kuhusu mada maalum ambayo una utaalamu au ambayo shirika lako linahusika. Makala hizi hukaguliwa na kuchapishwa kwenye gazeti.
  • Kufadhili mchakato wa utengenezaji wa makala yaliyomo, ambayo ni pamoja na utafiti, kutembelea  wakulima  na wataalamu, uandishi wa makala, uhariri na muundo wa gazeti.
  • Kuchangia gharama za uchapishaji wa gazeti. Hii pia inaweza kuwa ni kuongeza idadi ya nakala kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima katika mikoa inayolengwa.
  • Kupokea na kusambaza  magazeti  kwa wakulima ambao shirika lenu linafanya kazi pamoja, na kuwasaidia wakulima kujadili na kutumia habari zilizo katika gazeti hilo.
  • Kusambaza makala na maudhui kwenye taarifa za habari, mikutano na vikao vya wakulima, mabaraza yaliyopo, ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii.
  • Tafsiri au kutayarisha makala katika njia nyinginezo za mawasiliano kama vile redio na televisheni.
  • Kutoa maoni juu ya kile kinachofanya kazi na kinachohitaji kuboreshwa. Hii ni kupitia njia zetu za mawasiliano; barua, simu, ujumbe mfupi na barua pepe.

Kwa kufanya hivi, tutawawezesha wakulima wengi hasa wanawake na vijana kupata teknolojia bora na ushauri wa kiufundi ili kudhihirisha uwezo wao wa kuzalisha mazao, kupata masoko, fedha na kukuza biashara zao za kilimo na kujipatia kipato.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *