- Mifugo

AZOLA KWENYE KILIMO HAI NI TUNU

Sambaza chapisho hili

Azola ni majani au magugu ambayo huota sehemu yenye maji kwa wingi. Mmea huu umekua ukitumiwa zaidi na wafugaji kama chakula mbadala kwa kuku.

Majani haya huliwa na kuku yakiwa mabichi au yakivunwa na kuanikwa kisha kuchanganywa kwenye chakula cha kuku.

Azola hutumika kulisha mifugo mingine kama vile bata, ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kondoo, sungura na pia ni chakula kizuri kwa samaki wanaofugwa kwenye mabwawa kama vile kambale (african catfish), sato (tilapia).

Majani haya yanasifika kwa kuwa na virutubisho vingi protini, vitamins A & B12, amino asidi pamoja na madini mbalimbali ya kalishamu, potashiamu, magnesiamu, fosiforas.

Unawezaje kutumia Azola kama mbolea

  • Azola husambazwa shambani moja kwa moja mara baada ya kuvunwa kisha kuvurugwa/kuchanganya na udongo wakati wa kulima kama tunavyofanya samadi.
  • Vuna Azola kisha ianike kwenye kivuli ikishakauka isage ili kupata unga kisha weka kwenye mashina ya mimea au kama ni nyingi mwaga kwenye mtaro shambani ijichanganye na udongo.
  • Mara baada ya kuvuna iache ioze kisha changanya na mbolea kama samadi au mbolea ya kuku na weka kwenye kiroba kisha tumbukiza kwenye maji ijichuje upate ikiwa kimiminika. Endapo ikiwa nzito changanya na maji kiasi kisha tumia njia ya matone kuweka kwenye mimea au tumia bomba kunyunyuzia kwenye mimea.
  • Vuna azola ikiwa mbichi kisha weka majani yake chini ya shina la kila mmea.

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *