Mkulima Mbunifu (MkM) is a farmer information service based in Arusha, Tanzania, and implemented since July 2011 with support from Biovision Foundation, Switzerland and Biovision Africa Trust (BvAT), Nairobi, Kenya. MkM operates legally and administratively under Sustainable Agriculture Tanzania (SAT). MkM aims to provide information to smallholder farmers to enable them adopt improved sustainable agriculture technologies and practices. MkM…
Mifugo
Fahamu wadudu wasumbufu katika ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku ni moja ya sekta ambayo imekuwa na faida kwa wafugaji walio wengi, na hata watu ambao wanafanya shughuli nyinginezo, lakini bado hujishughulisha na ufugaji wa kuku. Pamoja na aina hii ya ufugaji kuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea wafugaji kipato kikubwa, bado inakumbwa na changamoto mbalimbali. Mojawapo ya changamoto hizo ni pamoja na uwepo…
Fahamu mikakati rahisi inayoweza kutumika ili kupanua mradi wa ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni ndege maarufu na ana-yefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Kwa nini ni vigumu kuongeza…
Zingatia utunzaji wa ndama anapozaliwa
Ndama mara anapozaliwa anahitaji kupewa maziwa ya mwanzo ya mama yake, maziwa haya hujulikana kama colostrum, na ataendelea kupatiwa maziwa haya kwa siku tatu hadi nne. Colostrum ina virutubishi vingi vya mwili kwani ina wingi wa vitamini na madini na ni kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. Zaidi; Toleo lijalo
Utajuaje kama mayai ya kuku yataanguliwa
Ni jambo jema kufahamu kama mayai yanayoatamiwa na kuku yataanguliwa yote au mangapi hayataanguliwa. Na kwa wanaototolesha vifaranga ni muhimu zaidi kwao kujua hali ya mayai inavyoendelea ndani ya kiangulio na kufahamu kama kuna tatizo linaweza kusababisha kifaranga ndani ya yai kufa. Pia kujua kama kuna mayai ambayo hayatapelekea kutotoa kifaranga na kuyaondoa. Hii yote hufanyika kwa kuyachunguza mayai yanayototolewa…
Fahamu afya ya mnyama ili kumkinga na magonjwa
Wanyama walio wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa msaada kwa wakati pale maradhi yanapowakumba. Katika Makala zilizopita tuliandika juu ya sifa za mnyama mwenye afya na katika toleo hili tumeona vyema kurudia kuchapisha mada hii ili kuwasaidia wafugaji wengi ambao mara nyingi wamekuwa wakipoteza wanyama kwa ghafla bila kujua tatizo limetokana na nini. Mfugaji mzuri anatakiwa kujua nini kwa…
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Ufugaji holela wa kuku haufai na ni hatari
Nimekuwa mfugaji wa kuku kwa kipindi cha miaka mingi sana, tatizo ni kwamba kuku wangu hawana banda maalumu na hukutana nao jioni tu wanapoingia jikoni, na kutoka asubuhi, nimesoma kidogo kwa jirani yangu aliekuwa na Mkulima mbunifu juu ya ufugaji wenye tija, je nikianza haitanigharimu sana kwa kuwa wao hujitafutia chakula wenyewe?-Haule, Iringa. Kuku kama ilivyo kwa mifugo wengine, wanahitaji…
Fahamu ugonjwa wa ukurutu na namna ya kuudhibiti
Ukurutu ni ugonjwa wa ngozi ambao huambukizwa kwa njia ya kugusana kati ya mnyama aliyeathiriwa na aliye mzima. Kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kwa jina la menji (Mange) na husababishwa na utitiri ambao kitaalamu wanaitwa mange mites. Wadudu hawa hujikita kwenye ngozi na kufanya ngozi kuwa ngumu kama yenye magaga, kumfanya mnyama kuwashwa na mwisho manyoya kupukutika na kuondoka kabisa.…