Ni muhimu kwa wafugaji kutumia makingo katika kuzalisha malisho aina ya nyasi na mikunde ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malisho bora na ya kutosha. Makingo hutengenezwa kwa kuchimba mitaro na kupanda majani kwenye mistari ya kontua. Makingo pia huweza kutengenezwa kwa kutumia mawe, takataka au mabaki ya shambani baada ya mavuno. Umuhimu wa makingo Makingo yanahitajika sana…
Mifugo
Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa
Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kisayansi kwa jina la Phlebovirus vya kabila la Bunyaviridae. Virusi hivi huenezwa na wadudu waumao hasa mbu wa aina ya Aedes, Anopheles, Culex, Mansonia nk. Ugonjwa huu huwapata ng’ombe, mbuzi, ngamia, kondoo na pia binadamu. Ugonjwa huu pia huwapata wanyamapori kama vile; swala, nyati na nyumbu. Njia…
Mambo machache muhimu ya kuzingatia kwa uzalishaji wa ng’ombe
Kuna aina nyingi za chanjo, na chanjo hizo zimegawanyika katika makundi mawili, chanjo hai na chanjo mfu. Chanjo mfu inabidi irudiwe kila mwaka au zaidi kulingana na aina ya ugonjwa. Chanjo hai huchomwa mara moja kwa mwaka au miaka mitatu kisha kurudiwa tena. Chanjo hizi hutolewa kwa ajili ya magonjwa yanayosababishwa na bakteria na virusi. Magonjwa menghine kama ECF hayana…
Nguruwe: Mifugo yenye gharama ndogo, tija zaidi
Kwa kawaida nguruwe ni lazima wafugwe ndani ya banda, wasiachwe kuzurura ovyo nje Ili kuwa na ufugaji wenye tija, na kuweza kuepuka baadhi ya magonjwa yanayoshambulia nguruwe, ni lazima mfugaji azingatie mambo ya msingi katika ufugaji. Banda Ni muhimu kuhakikisha kuwa unapohitaji kufuga nguruwe, unakuwa na banda lililotayarishwa vizuri na liwe imara. Utayarishaji mbaya wa banda unaweza kusababisha nguruwe kuugua…
Nawezaje kutunza g’ombe na kukabilina na magonjwa
Bila matunzo mazuri na kuzingatia kanuni za ufugaji, mfugaji hawezi kupata faida na kufikia malengo yake. Shauriana na wataalamu unapoona kuna jambo linalokutatiza Ufugaji hasa wa ng’ombe wa maziwa ni shughuli ambayo imejipatia umaarufu kwa kiasi kikubwa sana katika jamii mbalimbali, maeneo ya vijijini na hata mijini. Pamoja na shughuli hii kuwa maarufu na yenye faida, kuna changamoto mbalimbali zinazoambatana…
Wanahabari na Kilimo hai
Siku za hivi karibuni, mradi wa Mkulima Mbunifu uliratibu na kuendesha mafunzo ya kilimo hai kwa waandishi wa habari nchini Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tatu yalifanyika katika shamba la kilimo hai SJS- St Joseph Sustainable Organic Farm lililopo katika kijiji cha Kwanyange Wilaya ya Mwanga. Mafunzo haya yalifadhiliwa na shirika la Biovision (Bv) Foundation lililopo Switzerland. Katika mafunzo hayo…
Utunzaji bora wa majike ya nguruwe
Utunzaji bora wa majike ni muhimu kwani utamuwezesha mfugaji kupata mazao mengi na bora. Majike wazazi watunzwe vizuri ili kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa kwa mwaka na kuongeza faida kwa mfugaji. Utunzaji bora ni kiini cha idadi ya watoto watakaozaliwa,watakaoishi na Muda wataochukua kufikia uzito kuuza na gharama zitakazotumika. Kuchagua jike bora Mfugaji anashauriwa kuchagua nguruwe jike anayetegemewa kuwa mzazi…
Fahamu namna magonjwa makuu ya mifugo yanavyoambukizwa na namna ya kukabiliana nazo
Magonjwa ya mifugo ni moja kati ya matatizo yanayokabili maendeleo ya tasnia ya mifugo nchini. Kumekuwepo na kuenea kwa magonjwa ya mifugo nchini kama vile magonjwa ya mlipuko yasiyokuwa na mipaka, magonjwa yanayoenezwa na wadudu, magonjwa ya mifugo yanayoambukiza binadamu na magonjwa yanayojitokeza ambayo ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya tasnia ya mifugo. Kwa kuwasaidia wafugaji waweze kutunza afya ya…
Ufugaji wa kuku unainua pato la mkulima kwa haraka
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni ndege maarufu na anayefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Kwa nini ni vigumu kuongeza…
Ufugaji wa mbuzi hutegemea lishe sahihi
Ufugaji wa mbuzi ni moja ya miradi ya ufugaji rahisi lakini yenye changamoto nyingi ikiwa mfugaji hatazingatia maswala muhimu yanayohitajika kufuatwa kwa usahihi katika mradi huu hasa juu ya lishe. Kama mfugaji makini, hakikisha unafahamu namna na nini cha kulisha mbuzi ili uweze kufanya ufugaji wenye tija na utakaokupatia kipato sahihi kulingana na uzalishaji unaofanya. Baadhi ya vidokezo muhimu Kwa…