- Mifugo, Samaki

Uliza kuhusu samaki kama una changamoto unayopitia kwenye mradi wako

Sambaza chapisho hili

Kanyalo anauliza:Naomba kujua ni wakati gani ninatakiwa kubadili maji katika bwawa ikiwa maji ninayotumia ni ya kujaza?

Muda wa kubalisha maji kwa kawaida siwezi kusema moja kwa moja ni baada ya muda kadhaa ila naomba unielewe kuwa uchafukaji wa maji katika bwawa inategemea na utunzaji katika bwawa lako. Mfano; ukilishia vyakula ambavyo sio sahihi kwa samaki huenda ukalazimika ukabadilisha maji mara kwa mara.

Lakini kwa kawaida kama unafuata kanuni bora maji huwa hatubadilishi yote katika bwawa mpaka pale kutakapokuwa na uchafukaji uliokithiri.kinachofanyika ni kupunguza maji na kuongeza maji mapya unaweza kufanya hivi pindi utakapo ona bwawa lako kama ukijani umezidi sana ndani ya bwawa au harufu, Hapo sasa utaanza kunukuu takwimu na mwenendo wa ubadilishaji maji katika bwawa lako.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

4 maoni juu ya “Uliza kuhusu samaki kama una changamoto unayopitia kwenye mradi wako

    1. Habari, karibu mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako.

      Sisi tunatoa elimu tu wala hatuuzi mbegu lakini tukipata wanakouza tutakuunganisha nao ili uweze kununua.

      Karibu sana.

  1. nawashukuru sana mkulima Mbunifu kwa makala zetu mnazo nitumia kila mwezi nazifurahia sana, kwa kweli hapa ninapoishi nilikuwa na magazeti yangu ya mkulima mbunifu ya siku nyingi nilikuwa sijayatupa nilikuwa narudia kuyasoma mara kwa mara, lakini hivi karibuni yamepotea nikakasirika kweli. Ila nashukuru kwa kwa hii website yenu vitu vingi vinapatikana humu ndani, nawaomba msivifute viendelee kuwepo tu navipenda. NAOMBA KUULIZA SWALI. Mimi kwa sasa ni mfugaji wa samaki sato sina shida huko, ila natamani kupata elimu ya ufugaji wa kambare na jinsi ya kutotolesha vifaranga vya samaki? pia na kama kuna semina zenu mnazifanya sehemu mbali mbali hapa nchini tujuzane.Mimi naishi Dar, niwatakie kazi njema na kutokata tamaa ya kugawa fursa za ujasiliamali kwa watanzania wote, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee.

    1. Habari,
      Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida la Mkulima Mbunifu.

      Hongera sana kwa kuendelea kufanya shughuli za ufugaji wa samaki. Kuhusu ufugaji wa kambale na ufugaji wa aina yeyote ya samaki, tafadhali wasiliana na mtaalamu wa samaki Bw. Musa Saidi Ngametwa kwa simu namba 0718 986328/0753 971536 yeye yupo Dar ataweza kuwa msaada kwako.

      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *