- Mifugo

Namna ya kuwavutia nyuki kuingia mzinga mpya

Sambaza chapisho hili

Tatizo kubwa linalowakabili wakulima wanaotaka kuanzisha ufugaji wa nyuki ni mzinga mpya kukaa muda mrefu bila nyuki. Tatizo hili linapotokea ni vizuri kuzingatia yafuatayo;

  • Weka nta kwenye mizinga yako.
  • Weka mizinga yako katika hali ya usafi na kusiwe na wadudu. Nyuki hawapendi mzinga mchafu.
  • Hakikisha hakuna siafu wala panya wanaoishi kwenye mzinga.
  • Ning’iniza mzinga msimu ambao kuna makundi mengi ya nyuki yanayohama

Makundi ya nyuki huama wakati ambao nyuki wamezaliana kwa wingi na kuwepo malikia mwingine kwenye mzinga hivyo kusababisha kuhama ili kuunda kundi jingine. Msimu huo wa mgawanyiko ni rahisi nyuki kufanya makazi katika mzinga wako kwa haraka. Tafuta mahali pazuri pakuning’iniza mzinga wako. Kama haujui msimu wa makundi ya nyuki kuhama waulize wakulima wenzio wanaofuga nyuki katika eneo lako.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *