Ndugu msikilizaji na mfuatiliaji wa vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu/SAT, tunaomba radhi kutokana na kipindi chetu kilichokusudiwa kurushwa hewasi siku ya jumamosi tarehe 30 Oktoba 2021 kutokusikika. Hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Sasa kipindi hicho cha kilimo kilichokuwa kinahusu kilimo mseto na kilimo cha mzunguko wa mazao kitarushwa upya siku ya jumamosi ya tarehe…
Mazingira
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…
Gugu karoti lina madhara makubwa
Gugu karoti (Parthenium hysterophorus) ni mmea vamizi ambao una madhara mengi kwa binadamu, mazao, wanyama au mifugo pamoja na kuharibu uoto wa asili. Gugu hili lina madhara mengi kama; Muwasho unaoweza kusababisha kujikuna na kupata malengelenge, ugonjwa wa pumu ukivuta vumbi lake, muwasho wa macho, mnyama kupasuka na kuvimba midomo kama akila majani. Aidha gugu karoti husababisha maziwa ya ng’ombe…
Madhara yatokanayo na uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO uchafuzi wa mazingira husababisha takribani vifo milioni saba (7) kila mwaka, na kusababisha ulemavu kwa watu wanaoishi na magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa hewa. Nini sababu za uchafuzi wa hali ya hewa Uchafuzi wa hewa husababishwa na gesi na chembechembe zinazoruhusiwa kuingia angani kupitia shughuli mbalimbali za kibinadamu. Miongoni mwa shughuli…
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea
Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu. Hii ni hali ya kimaumbile katika kusawazisha idadi. Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuzidi idadi na kusababisha madhara. Madhumuni ya njia ya kiasili…
Utengenezaji wa mbolea ya mboji kwa mazao ya kilimo hai
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Vipande vya vitu au sehemu za viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda…
Fahamu udongo wako ili kuboresha uzalishaji wa mazao
Kuna virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ukuaji wa mmea. Upungufu wa mojawapo ya virutubishi hivi muhimu utapunguza ukuaji wa mimea. Mavuno yanategemea kiwango cha virutubisho muhimu kwa mmea vipatikanavyo katika udongo. Mimea yote hutegemea vitu muhimu kukua vizuri. Vitu hivi vinaweza kugawanywa katika makundi mawili; Vitu vya madini, kupitia udongo. Vitu visivyo vya madini: haidrojeni, oksijeni, na kaboni ambazo zinapatikana kwa…
Kilimo mseto huongeza uzalishaji wa mazao, malisho na utunzaji wa mazingira
Mara nyingi wafugaji wa mbuzi na wanyama wengine huendesha shughuli za kilimo, katika mashamba yao kwa kuotesha mimea ya aina mbali mbali. Hii ni pamoja na miti malisho. Kilimo mseto ni mfumo wa kilimo wa kuchanganya miti na mazao katika shamba moja. Miti sahihi kwa kilimo mseto humnufaisha mfugaji kwa njia nyingi. Miti hiyo huweza kutumiwa kama malisho ya mifugo.…