- Kilimo, Mimea, Udongo

Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea

Sambaza chapisho hili

Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu. Hii ni hali ya kimaumbile katika kusawazisha idadi.

Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara kwenye mimea.

Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuzidi idadi na kusababisha madhara. Madhumuni ya njia ya kiasili nikujaribu kuweka uwiano katika mazingira. Mfumo huu haujanuiwa kuangamiza wadudu bali kuwakabili.

Iwapo mimea itashambuliwa, ni vigumu kudhibiti hasara. Ni bora basi kuchukua tahadhari na kuzuia.

Dawa ya kiasili ni bora kuliko zile za kemikali?

Madawa ya kemikali sio suluhisho la shida ya magonjwa na wadudu.

Matumizi ya kemikali yameimarika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita ilihali idadi ya magonjwa na wadudu imezidi. Zifuatazo ni faida zinazothibitisha umuhimu wa njia za kiasili.

Gharama

Gharama ni kidogo ikilinganishwa na madawa ya kemikali. Viungo vinavyohitajika hupatikana kwa urahisi pasipo gharama au fedha. Viungo hivi vyaweza kupatikana shambani.

Usalama kwa binadamu

Matumizi ya kemikali yanaweza kudhuru afya ya binadamu. Madhara yaweza kutokana na kule kutofahamu maelezo ya matumizi. Aidha, maelezo yaweza kuandikwa kwa lugha isiyofahamika na mtumiaji.

Matokeo yake madawa haya yamesababisha hasara ya ngozi, maumivu ya kichwa na hata saratani ya ngozi. Kila mwaka, milioni moja ya watu huathiriwa kwa sumu itokanayo na madawa ya kemikali.

Kati ya idadi hii, watu 20,000 hufariki. Vifo hivi hutokea katika nchi zinazostawi mahali matumizi ya aina Fulani ya kemikali zilizopigwa marufuku Uingereza na Amerika hutumiwa.

Usalama kwa mazingira

Dawa za kemikali katika kukabili wadudu na magonjwa huathiri mazingira kwa njia zifuatazo:

  • Huua wadudu wenye manufaa.
  • Dawa za kemikali zaweza kubakia kwenye mazingira na miili ya wanyama na kusababisha maafa siku za usoni.
  • Wadudu na magonjwa huweza kuhimili dawa hizi baada ya kizazi fulani, hivyo basi kufifisha nguvu za kemikali dhidi yao na kujenga usugu dhidi ya kemikali hizo.

Je unawezaje kukabili wadudu na magonjwa

Tambua shida

Kabla ya kukabili magonjwa au wadudu, nibora kufahamu na kutambua shida ilioko. Unapofahamu na kuta-mbua shida, waweza kutofautisha aina ya madhara. Aidha, ni hali ya hewa, upungufu wa madini au mago-njwa yaliyosababishwa na wadudu. Kutambua shida hupelekea kuka-bili au kuzuia matatizo.

Udongo wenye rutuba

Udongo uliohifadhiwa kwa mfumo hai huimarisha viwango vya rutuba. Mimea yenye afya huweza kuhimili magonjwa na wadudu. Ni muhimu kutunza na kuimarisha rutuba ya udo-ngo. Madhumuni ya kutunza udongo ni;

  1. Kuimarisha rutuba (viumbe hai) kwenye udongo.
  2. Lishe kwa viumbe walio kwenye udongo.
  3. Kuipatia mimea madini yana-yofaa.

Ijapokuwa kemikali huimarisha afya ya mimea, matumizi yake yaweza kuwa na madhara. Mmea waweza kuwa na kiasi kikubwa cha nitrojeni itokanayo na kemikali na kuufanya uvutie wadudu. Imebainika kwamba wadudu hutaga mayai mengi katika sehemu zilizo na mimea yenye nitrojeni nyingi ukilinganisha na mimea iliyopandwa kwa njia ya kiasili.

Mimea yenye afya

Mimea yenye afya huweza kuhimili wadudu na magonjwa. Aina ya mimea pia huzuia wadudu au magonjwa. Mmea unaokuzwa katika sehemu isiyohitajika huweza kushambuliwa kwa urahisi.

Ni vyema kuzingatia aina ya udo-ngo, hali ya hewa, muinuko, rutuba na maji wakati wa kupanda. Mimea huwa na afya na kuhimili magonjwa na wadudu iwapo sehemu inafaa.

Katika kuimarisha afya, utahitajika kupalilia ili kuondoa ushindani kati ya mimea na kwekwe.

Mzunguko wa mimea kwa zamu

Upanzi wa mmea wa aina moja kila baada ya msimu waweza kuongeza uwepo wa wadudu na magonjwa. Magonjwa haya hubakia kwenye udongo na hujitokeza kila msimu. Kukabili shida hii, ni bora kuzingatia mfumo wa mzunguko wa mazao kuruhusu kurejelea aina fulani ya mmea katika sehemu baada ya miaka 3 au 4.

Mzunguko wa mimea kwa zamu katika kipindi cha miaka 4 hujumuisha mahindi na maharagwe, nafaka na mboga za mizizi na kati ya mimea ifuatayo;

  1. Konde la nyasi au kichaka (muda fulani bila kupanda mimea).
  2. Jamii ya mikunde. Mimea ya jamii hii hukuzwa kutoa mbolea ya kijani na kuimarisha rutuba.

Katika bustani ya mboga, upanzi wa sukuma wiki au kabichi na vitunguu kila baada ya msimu, huongeza idadi ya magonjwa na wadudu. Unapo-vunja mzunguko utasaidia kukabili magonjwa na wadudu.

Afya bora

Iwapo utaacha mimea iliyoathiriwa kwenye bustani, magonjwa au wadudu huenea kwengineko. Mabaki ya mimea iliyoathiriwa yapaswa kuondolewa na kuharibiwa. Waweza kutengeneza mboji ukitumia mabaki hayo. Mboji inapooza huvunjilia mbali baadhi yamagonjwa na wadudu. (Maelezo ya ziada kuhusu mboji yaweza kupatikana kutoka kwa HDRA). Iwapo utashuku madhara kutokana na mabaki hayo, ni bora kutahadhari kwa kuchoma.

Jinsi ya Kulima

Baadhi ya wadudu hubakia kwenye udongo. Kulima nyakati za kiangazi huharibu na kukausha ngome zao na hata kuua wadudu wachanga. Vilevile, ndege na wanyama wengine huchakura na kuwaua wadudu waka-ti wa kutayarisha shamba. Mfumo wa kulima pia waweza kuzika wadudu chini na kuwaangamiza. Tahadhari yapaswa kuchukuliwa wakati wa-kulima ili kuzuia mmonyoko wa udongo.

Aina ya Udongo

Kiasi cha tindikali ya udongo huathiri magonjwa na wadudu. Hitilafu ya tindikali huweza kuathiri wadudu na magonjwa.

Kwa mfano magonjwa ya viazi (potato scab) huzuiwa kwa tindikali iliyokolea chini ya 7. Kuimarisha tindikali katika eneo hili, waweza kuongeza nyasi na majani kwenye mitaro katika bustani ya viazi.

Magonjwa ya (club root) hayana madhara katika sehemu iliyo na upungufu wa tindikali chini ya 7. Hivyo basi waweza kutumia jivu na chokaa ili kuyeyusha tindikali.

Maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.gardenorganic.org

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *