Mazingira

- Kilimo, Mimea, Udongo

Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea

Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu. Hii ni hali ya kimaumbile katika kusawazisha idadi. Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuzidi idadi na kusababisha madhara. Madhumuni ya njia ya kiasili…

Soma Zaidi

- Kilimo, Udongo

Utengenezaji wa mbolea ya mboji kwa mazao ya kilimo hai

Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Vipande vya vitu au sehemu za viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda…

Soma Zaidi

- Mazingira, Udongo

Fahamu udongo wako ili kuboresha uzalishaji wa mazao

Kuna virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ukuaji wa mmea. Upungufu wa mojawapo ya virutubishi hivi muhimu utapunguza ukuaji wa mimea. Mavuno yanategemea kiwango cha virutubisho muhimu kwa mmea vipatikanavyo katika udongo. Mimea yote hutegemea vitu muhimu kukua vizuri. Vitu hivi vinaweza kugawanywa katika makundi mawili; Vitu vya madini, kupitia udongo. Vitu visivyo vya madini: haidrojeni, oksijeni, na kaboni ambazo zinapatikana kwa…

Soma Zaidi

- Mazingira

Mkaa wa pumba za mchele na matumizi yake

Mkaa wa pumba za mchele hutengenezwa kwa kuchomwa kwa njia maalumu ya kisayansi asilia. Mkaa huchomwa na kuwa na rangi moja ya kikaboni (rangi nyeusi) iliyoiva vyema. Ndani ya mkaa huu kuna madini ya fosiforasi, potasi, kalshiam, magnesiam, na virutubisho vingi vya asili vinavyohitajika kwa ajili ya kupanda mazao. Mkaa huu unaweza kutumika kama sehemu mojawapo ya chakula cha nguruwe…

Soma Zaidi

- Mazingira

Matumizi ya samadi ya wanyama na mimea kwenye kilimo hai

Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni. Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho. Samadi iliyo tayari kwa matumizi Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mazingira

Madhara ya kiafya kutokana na viuatilifu

Wakulima wengi wamejisababishia madhara ya kiafya kutokana na matumizi ya viuatilifu. Hii ni kutokana na kutokua na maarifa sahihi na kutokutumia hatua zinazostahili za kinga au kutekeleza mbinu sahihi za udhibiti. Viuatilifu vya kiwandani na zana zake kwa kawaida huhifadhiwa majumbani ambako kuna hatari ya kugusana na chakula na watoto. Pia mazao yaliyopuliziwa dawa wakati mwingine huvunwa bila ya kuzingatia…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mazingira, Mimea

Rutuba ya udongo ndio uhai wa udongo na tija kwa mkulima

Ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha anauilisha udongo kwa kutumia virutubisho vya asili, ili kuweza kuwa na rutuba na kuzalisha mazao yenye tija. Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho. Vipengele…

Soma Zaidi