- Kilimo, Udongo

Mbinu za uhifadhi wa udongo wa kilimo na mimea

Sambaza chapisho hili

Udongo ni sehemu kubwa ya kilimo. Tunaweza kusema bila udongo hakuna kilimo lakini bila bila udongo wenye rutuba hakuna mavuno bora.

Mara nyingi mvua, upepo na matumizi ya mbolea za viwandani, uharibifu wa mazingira kama kukata miti, wanyama n ahata shughuli zingine za kibinadamu ndiyo hupelekea kuharibika kwa udongo.

Kuna njia nyingi za zinazotumia kilimo za kuhifadhi udongo na maji na kuzuia uharibifu wa udongo.

Mbinu za uhifadhi wa kilimo na mimea hujumuisha matumizi ya mimea na mitindo ya ukulima yanayoweza kufanywa kulinda na kuhifadhi udongo na maji.

  1. Utunzaji wa mimea

Utunzaji bora wa mimea hupunguza mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na maji na upepo hata ukafikia kiwango kinachokubalika na kuimarisha rutuba. Katika mbinu hii mkulima anashauriwa kuchagua mazao yanayofaa kulingana na udongo na mteremko kisha kupanda mapema kwa kutumia mifumo sahihi ya upandaji au ubadilishaji wa mazao huku akihakikisha udongo umefunikwa.

  1. Mbinu za ukulima

Ukulima hulenga kuimarisha hali halisi ya kibaiolojia ya udongo kwa uzalishaji wa mazao kwa kuhakikisha uandaaji wa vitalu mapema, upandaji na udhibiti wa magugu. Mkulima anashauriwa kutumia mbinu ya ukulima ambayo haifanyi udongo wa juu kulainika lakini pia kuvunjavunja udongo mgumu pale inapohitajika kufanya hivyo.

  1. Matumizi ya mbolea

Mkulima anatakiwa kuongeza samadi au mbojia katika udongo ili kuleta virutubishi vya mimea vinavyohitajika kwa ukuaji wa haraka na kuifanya mimea kufunika udongo na kuunginga na mmomonyoko kisha kuwezesha maji kupenya ardhini na kupelekea mavuno mengi zaidi.

  1. Kilimo cha miti

Kilimo cha miti hujumuisha kupanda au kihifadhi miti ambayo tayari iko shambani kwa lengo la kuhifadhi udongo. Miti hupunguza ngu ya matne yam aji kushukia kwenye udongo lakini pia mizizi hushikamanisha udongo.

Miti pia hufunika udongo, hupunguza kiwango cha joto, hupunguza mtiririko wa maji juu ya ardhi pamoja na nguvu ya upepo. Miti hurudisha virutubishi kutoka udongo wa chini na kupeleka kwenye mimea jamii ya mikunde ambayo nayo huzalisha na kudumisha naitrojeni kisha kunufaisha mazao mengine ya chakula.

  1. Kilimo cha kontua

Ukulima wa kontua hujumuisha kulima, kupanda na kupalilia kwa kufuata kontua ya upande hadi upande wa mteremko na siyo juu chini. Ukulima huu husaidia kupunguza mmomonyoko wa udongo katika mashamba yenye mteremko.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *