- Binadamu

Afya ya mwili hutengenezwa na ulaji wa chakula unaofaa wa kila siku

Sambaza chapisho hili

Chakula kinachofaa tunamaanisha ulaji unaofaa ambao ni ulaji wa chakula mchanganyiko, cha kutosha na chenye virutubisho vyote kwa uwiano unaotakiwa.

Ulaji unaofaa ni lazima uzingatie matumizi ya mafuta kwa kiasi kidogo sana. Mafuta ya nyama sio mazuri kwani yanahusishwa na magonjwa ya moyo, badala yake inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea kama vile alizeti.

Matumizi ya sukari na chumvi pia yasizidi kiwango, yawe ya kiasi tun a kwa wale wanaokunywa pombe wanywe kwa kiasi tu ama waache kabisa.

Kula chakula mchanganyiko
Ulaji wa chakula mchanganyiko hukuwezesha kupata virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini, kwa mfano vyakula vya wanga vinasaidia kuupa mwili nguvu na joto, mwili husaidia kujenga mwili, vitamini na madini hulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Kila siku jitahidi kula vyakula kutoka katika makundi yafuatatyo:

  • Vyakula vya asili ya nafaka, ndizi za kupika na mizizi.
  • Vyakula vya jamii ya kunde, asili ya wanyama na mbegu za mafuta.
  • Mboga mboga.
  • Sukari, asali na mafuta.

Kutokula mafuta mengi
Mafuta mengi mwilini hasa yale yenye asili ya wanyama yanaweza kusababisha ongezeko la magonjwa ya moyo na shinikizo kubwa la damu, hivyo inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea.

Jinsi ya kupunguza mafuta:

  • Tumia mafuta kidogo wakati wa kupika.
  • Epuka kula vyakula vilivyokaangwa kwa mafuta badala yake chemsha, oka au choma.
  • Punguza mafuta kwenye nyama iliyonona, na ikibidi ondoa ngozi ya kuku kabla ya kupika.
  • Chagua nyama au samaki wasio na mafuta mengi.

Kula matunda na mbogamboga kwa wingi
Vyakula hivi huupatia mwili kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile baadhi ya magonjwa ya moyo, saratani na kisukari.

Matunda ni chanzo cha virutubisho/viinilishe vya vitamini na madini ambavyo hupatikana kwa wingi kuliko kwenye vyakula vingine. Kula matunda si chini ya mara mbili kwa siku.

Faida za virutubisho hivi ni pamoja na;

  • Huifanya ngozi kuwa ng’aavu na yenye afya na vidonda kupona vizuri.
  • Huwezesha macho kuona vizuri.
  • Husaidia kuimarisha ufahamu.
  • Husaidia uyeyushaji wa vyakula tumboni na kufyonza madini mwilini.
  • Hutumika katika kutengeneza damu.
  • Husaidia katika uundaji wa chembe za uzazi.

Virutubisho hivi havihifadhiki katika mwili wa binadmu hivyo ni vizuri matunda tofauti yajumlishwe kwenye mlo/milo ya siku.

Kwa upishi wa mboga, pika kwa muda mfupi ili kupunguza upotevu wa vitamini na madini na tumia maji kidogo wakati wa kupika. Maji yanayopikia mboga yaendelee kutumika na sio kumwagwa

Vyakula vyenye nyuzinyuzi
Vyakula vya nyuzinyuzi (Fibre) husaidia katika usagaji wa chakula tumboni na pia huweza kupunguza baadhi ya saratani, magonjwa ya moyo na kisukari.

Ili kuongeza nyuzinyuzi;

  • Kula saladi na matunda mara kwa mara.
  • Kula tunda zima badala ya juisi.
  • Tumia unga usiokobolewa dona.
  • Kula vyakula vya jamii ya kunde mara kwa mara kwani zina nyuzinyuzi kwa wingi.

Punguza Chumvi

Tumia chumvi kidogo wakati wa kupika na epuka vyakula vyenye chumvi nyingi kama vile bisi, viazi vya kukaushwa (crips).

Epuka uongezaji wa chumvi kwenye vyakula kama vile kwenye mihogo ya kuchoma, matunda kama maembe viazi vya kukaanga (chips) na badala yake unaweza kutumia viungo kama ndimu na pilipili kuongeza ladha.Punguza sukari
Sukari huongeza nishati mwilini, hivyo huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya sukari pia huzalisha bacteria kinywani ambao husababisha karisi (meno kutoboka).

Hivyo inashauriwa;

  • Kunywa vinywaji ambavyo havina sukari kama vile madafu na juisi za matunda badala ya soda zenye sukari.
  • Kama unatumia sukari, tumia kiwango kidogo.
  • Punguza kula vitu vyenye sukari nyingi kama keki, pipi, chocolate, ice.
  • Punguza matumizi ya vyakula vilivyoongezwa sukari.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Afya ya mwili hutengenezwa na ulaji wa chakula unaofaa wa kila siku

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *