Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…
Mifugo
Je, unafahamu kuwa kilimo hai kinalipa
Bonyeza hapo juu kusikiliza kuhusu kilimo hai
Ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine
Katika toleo lililopita tuliangalia utangulizi wa mada hii ya ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine. Tuliweza kuangazia mambo kadha wa kadha muhimu, na miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na faida za ufugaji huo, pamoja na manufaa ya ufugaji wa namna hiyo; Aina ya samaki wanaofaa katika kilimo mseto Perege na Kambale ni samaki wanaofugwa katika maeneo mabalimbali nchini…
Umuhimu wa kuotesha malisho kukabili ukame
Malisho yaliyo mengi hapa nchini ya asili ambayo hutegemewa na mifugo hukomaa na kukauka mapema zaidi na hivyo kusababisha lishe kwa wanyama kuwa duni wakati wa kiangazi ambapo wanyama huhangaika sana kupata chakula. Kutokana na upungufu huo ni vyema wafugaji kuotesha aina mbalimbali za malisho bora ili kunusuru mifugo yao wakati wa ukosefu wa chakula katika malisho ya asili. Mfugaji…
Jinsi ya kutega nyuki wakubwa kuingia kwenye mzinga
Ufugaji wa nyuki ni moja ya miradi mikubwa inayofanywa na wafugaji wengi kwa lengo la kujipatia kipato. Ufugaji huu umekuwa ukihusisha ufugaji wa nyuki wadogo na wakubwa kupta asali, nta, sumu pamoja uuzaji wa mizinga. Wafugaji wengi wamekuwa wakikwama kupata nyuki katika mizinga yao pindi wanapokamilisha utengenezaji wa mizinga kutokana na kukosa maarifa ya utegaji nyuki ili waingie ndani ya…
EMAS: Kirutubishi chenye matumizi mengi kwa mkulima
Mlima bora ni yule anayetumia malighafi sahihi ili kuzalisha mazao mengi yenye tija na salama kwa chakula. EMAS ni nini? EMAS Effective Micro Organisms Active Solution ni namna nyepesi ya kutengeneza bakteria wazuri ama rafiki kwa njia ya kimiminika ambacho ni rahisi kutumia na pia ni salama. Mahitaji Maziwa Fresh lita 10 Maji ya mchele lita moja Molasesi lita 10…
Ukisoma jarida la Mkulima Mbunifu kila siku utakuwa na tabasamu usoni mwako
Hebu waangalie wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu wakifurahia kupata nakala zao
Uzalishaji wa malisho
Bonyeza hapa na sikiliza kuhusu malisho aina ya matete na faida zake