Kabla ya kusindika vitunguu saumu ni muhimu kuhakikisha kuwa vitunguu vinavyosindikwa vimekomaa vizuri na vipo kwenye kiwango cha ubora na havijaoza. Dalili za vitunguu saumu vilivyokomaa Vitunguu saumu huwa tayari kuvunwa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano tangu kusia mbegu Vitunguu saumu vilivyokomaa huonyesha majani kunyauka na kubadilika rangi na kuwa ya manjano hadi kahawia. Shingo ya vitunguu saumu…
Binadamu
Mbolea hai na madawa ya asili ni muhimu kwa mimea, wanyama na binadamu
Mkulima anapotumia mbolea za viwandani na kemikali kwa muda mrefu, ni dhahiri kuwa udongo hudhoofika na kushindwa kuzalisha. Afya yake pia ipo mashakani kwa kuwa kemikali zina madhara makubwa sana. Kilimo ni lazima kuwezesha na kuongeza afya ya udongo, mimea, wanyama na binadamu. Udongo ni nguzo muhimu katika maisha ya viumbe wote kwa ujumla. Udongo ulioharibiwa hauwezi kuzalisha chakula vizuri,…
Je wajua kuhusu mti wa Mlonge (Moringa)
Moringa (Moringa spp.) maarufu kama mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kwa matumizi ya binadamu, wanyama na hata katika kutengeneza virutubishi kadhaa. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji. Faida na matumizi ya mti wa Moringa 1.Virutubishi Faida na matumizi ya mti wa MoringaKaribu kila …
Ujue ubuyu na faida yake katika mwili wa binadamu
Ubuyuni tunda ambalo hupatikana katika miti jamii ya Adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbalimbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia ili kuongeza ladha wengine huchanganya ubuyu na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha ya ubuyu. Ubuyu umekuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu. Ni tunda la asili na linapatikana porini hasa katika kanda kame (Semi arid).…
Jua matokeo ya lishe duni kwa watoto na jinsi ya kuboresha afya
Kila mwaka, watoto wengi chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufa kwa sababu ya chakula duni na kisichotosha. Watoto hawa hawapati chakula chenye vitamini, madini ya iodini na chuma ambayo yanahitajika kwa afya na ukuaji mzuri. Hali hii inasababisha utapiamlo. Utapiamlo unamaanisha upungufu, kupita kiasi, au kukosa usawa katika ulaji wa vyakula na virutubishi muhimu mwilini. Aina mbali mbali za…
Madhara ya utupaji holela wa makopo ya viuatilifu
Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka mwanadamu na viumbe hai katika maisha yao. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako. Mazingira yakiwa katika hali ya usafi hupendeza na kuvutia. Mazingira yasipowekwa katika hali ya usafi huatarisha afya ya viumbe hai waishio katika mazingira hayo ikiwamo binadamu, wanyama, na mimea pia. Pamoja na serikali kutangaza kukataza matumizi ya mifuko ya…
Fahamu faida za lishe ya samaki kwa watu wazima na watoto
Watu wanaoishi kwa kutegemea vyakula vya kwenye maji huishi kwa muda mrefu na huwa na kumbukumbu nzuri na uwezo mkubwa wa kufikiri. Katika matoleo kadha wa kadha ya jarida la MkM, tumekuwa tukieleza kwa ufasaha kabisa namna ya ufugaji bora wa samaki, na faida zake kiuchumi kwa mfugaji na jamii kwa ujumla. Katika toleo hili, tumeona ni vyema kuwa na…
Gusa bomba: Njia salama ya kunawa mikono
Gusa bomba ni teknologia inayokuwezesha kusafisha mikono yako bila kugusa chanzo cha maji. Kwa kawaida tumezoea kuwa unaenda bombani kunawa mikono kabla ya kula chakula, baada ya kutoka chooni, au wakati wowote unapohisi kuchafuka. Unapofika kwenye bomba huku mikono yako ikiwa michafu, unafungua bomba, maji yanatoka halafu unanawa mikono. Baada ya kumaliza kunawa mikono unafunga bomba. Wakati wa kufunga bomba,…
Jifunze kusindika nazi na kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali
Kusindika nazi Katika msimu huu, nazi zinapatikana kwa wingi mashambani na sokoni na hivyo kufanya gaharama za uuzaji kuwa chini kidogo. Hata hivyo pamoja na upatikanaji huu, wakulima na wauzaji wengi hawajafikiria namna ya kuongezea thamani zao hili ili kuzalisha bidhaa bora zaidi zenye soko na muda mrefu wa matumizi. Mkulima Mbunifi unashauri kusindika nazi na kuzalisha bidhaa hizo ili…
Ijue teknolojia ya vijidudu vidogo vidogo na matumizi yake katika kilimo
Kumekuwa na changamoto kadhaa za kwenye kilimo ikiwemo kukosekana na rutuba magonjwa na wadudu waharibifu. Teknolojia ya EM imekuwa ikitumiwa nchi mbali mbali duniani na pia Tanzania. Baadhi ya maeneo ya ardhi hayana rutuba kutokana na mambo kadhaa kama vile kulimwa kwa muda mrefu au matumizi ya mbolea za viwandani. Ingawaje mbolea za viwandani zinasaidia kuongeza rutuba, lakini ni…