Binadamu

- Binadamu

Imarisha afya ya mifupa kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali za kilimo hai

Mifupa yetu inarekebishwa kila wakati na tishu za mfupa zinavunjwa na kujengwa mara kwa mara. Uzani wa mfupa kawaida huongezeka hadi wakati wa utu uzima, lakini baada ya hapo, shida inaweza kukupata. Mifupa huupa mwili mwonekano sahihi, hulinda viungo vya ndani ya mwili (mfano Fuvu linalinda ubongo na kifua na mbavu zinalinda mapafu), hukusaidia kutembea, hutunza madini muhimu ya mwili…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo, Mimea, Redio, Usindikaji

Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu

Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo, Mimea, Redio, Usindikaji

Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo

Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…

Soma Zaidi

- Binadamu

Ubuyu na faida zake katika mwili wa binadamu

Ubuyu ni tunda ambalo hupatika­na kwenye miti jamii ya Adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbali-mbali wengi tukiutumia kama ma­tunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia kuongeza ladha kwenye vyakula. Ubuyu umekuwa tunda lenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu. Ni tunda la asili na linapatikana porini hasa katika kanda kame (semi-arid). Vitu vyote vilivyomo kwenye ubuyu vinatumika…

Soma Zaidi

- Binadamu

Vyakula muhimu katika mwili wa binadamu

Binadamu tunatumia misuli na ubongo kufanya kazi zetu za kila siku hivyo, tunahitaji kuweka miili katika hali nzuri. Ili mwili uwe na nguvu,kinga ya kutosha na i kuwa tayari kufanya kazi kwa kiwango cha juu ni lazima kula vizuri.. Kula vyakula vyenye virutubisho huboresha kiwango chako cha afya na nguvu mwilini. Inashangaza kwamba njia tunayotumia kupika vyakula huleta athari kubwa…

Soma Zaidi

- Binadamu

Fahamu vitamini na madini za kujenga kinga ya mwili

Vitamini na madini yanafanya kazi ya kujenga kinga ya mwili, na yanapatikana katika mboga na matunda. Ni muhimu kwa makundi ya watu kama watoto, mama wajamzito, mama anaenyonyesha na wazee, kwani huzuia na kusaidia kupambana na maambukizi ya magonjwa. Watu wengi hawali chakula cha kutosha chenye mboga na matunda, pamoja na vyakula vingine ambavyo ni vyanzo vya vitamini na madini.…

Soma Zaidi

- Binadamu

Fahamu faida za maji katika mwili wa mwanadamu

Maji ni uhai na bila maji, vitu vilivyo hai duniani haviwezi kuishi. Binadamu, mimea na wanyama wanahitaji maji safi ili kuwa na afya nzuri hivyo tunapaswa kuhakikisha tunatumia maji safi ya kunywa, kupika na hata kwa wanyama na mazao. Imekuwa kawaida kuona watu wakitembea na chupa za maji ya kunywa. Mbali na hali ya hewa kuwa na joto, umewahi kujiuliza…

Soma Zaidi

- Binadamu, Usindikaji

Sindika maziwa kuongeza pato na uepuke hasara

Kabla ya kusindika maziwa ya mgando au mabichi ni lazima kufanya vipimo vya awali ili kujua kama maziwa yanafaa kusindika au hayafai. Kipimo kikubwa kinachotumika kupima maziwa ni alkoholi (Ethanol) Kipimo hiki hutumika kutambua maziwa yaliyoharibika na maziwa yaliyoanza kuganda. Namna ya kupima Chukua kiwango kinacholingana cha Alkoholi (ethanol) na maziwa mabichi kisha changanya pamoja kwa kuweka katika chombo maalum…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo

Usindikaji wa vitunguu saumu

Kabla ya kusindika vitunguu saumu ni muhimu kuhakikisha kuwa vitunguu vinavyosindikwa vimekomaa vizuri na vipo kwenye kiwango cha ubora na havijaoza. Dalili za vitunguu saumu vilivyokomaa Vitunguu saumu huwa tayari kuvunwa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano tangu kusia mbegu Vitunguu saumu vilivyokomaa huonyesha majani kunyauka na kubadilika rangi na kuwa ya manjano hadi kahawia. Shingo ya vitunguu saumu…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Mifugo

Mbolea hai na madawa ya asili ni muhimu kwa mimea, wanyama na binadamu

Mkulima anapotumia mbolea za viwandani na kemikali kwa muda mrefu, ni dhahiri kuwa udongo hudhoofika na kushindwa kuzalisha. Afya yake pia ipo mashakani kwa kuwa kemikali zina madhara makubwa sana. Kilimo ni lazima kuwezesha na kuongeza afya ya udongo, mimea, wanyama na binadamu. Udongo ni nguzo muhimu katika maisha ya viumbe wote kwa ujumla. Udongo ulioharibiwa hauwezi kuzalisha chakula vizuri,…

Soma Zaidi