Moringa (Moringa spp.) maarufu kama mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kwa matumizi ya binadamu, wanyama na hata katika kutengeneza virutubishi kadhaa. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji. Faida na matumizi ya mti wa Moringa 1.Virutubishi Faida na matumizi ya mti wa MoringaKaribu kila …
Binadamu
Ujue ubuyu na faida yake katika mwili wa binadamu
Ubuyuni tunda ambalo hupatikana katika miti jamii ya Adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbalimbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia ili kuongeza ladha wengine huchanganya ubuyu na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha ya ubuyu. Ubuyu umekuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu. Ni tunda la asili na linapatikana porini hasa katika kanda kame (Semi arid).…
Jua matokeo ya lishe duni kwa watoto na jinsi ya kuboresha afya
Kila mwaka, watoto wengi chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufa kwa sababu ya chakula duni na kisichotosha. Watoto hawa hawapati chakula chenye vitamini, madini ya iodini na chuma ambayo yanahitajika kwa afya na ukuaji mzuri. Hali hii inasababisha utapiamlo. Utapiamlo unamaanisha upungufu, kupita kiasi, au kukosa usawa katika ulaji wa vyakula na virutubishi muhimu mwilini. Aina mbali mbali za…
Madhara ya utupaji holela wa makopo ya viuatilifu
Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka mwanadamu na viumbe hai katika maisha yao. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako. Mazingira yakiwa katika hali ya usafi hupendeza na kuvutia. Mazingira yasipowekwa katika hali ya usafi huatarisha afya ya viumbe hai waishio katika mazingira hayo ikiwamo binadamu, wanyama, na mimea pia. Pamoja na serikali kutangaza kukataza matumizi ya mifuko ya…
Fahamu faida za lishe ya samaki kwa watu wazima na watoto
Watu wanaoishi kwa kutegemea vyakula vya kwenye maji huishi kwa muda mrefu na huwa na kumbukumbu nzuri na uwezo mkubwa wa kufikiri. Katika matoleo kadha wa kadha ya jarida la MkM, tumekuwa tukieleza kwa ufasaha kabisa namna ya ufugaji bora wa samaki, na faida zake kiuchumi kwa mfugaji na jamii kwa ujumla. Katika toleo hili, tumeona ni vyema kuwa na…
Gusa bomba: Njia salama ya kunawa mikono
Gusa bomba ni teknologia inayokuwezesha kusafisha mikono yako bila kugusa chanzo cha maji. Kwa kawaida tumezoea kuwa unaenda bombani kunawa mikono kabla ya kula chakula, baada ya kutoka chooni, au wakati wowote unapohisi kuchafuka. Unapofika kwenye bomba huku mikono yako ikiwa michafu, unafungua bomba, maji yanatoka halafu unanawa mikono. Baada ya kumaliza kunawa mikono unafunga bomba. Wakati wa kufunga bomba,…
Jifunze kusindika nazi na kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali
Kusindika nazi Katika msimu huu, nazi zinapatikana kwa wingi mashambani na sokoni na hivyo kufanya gaharama za uuzaji kuwa chini kidogo. Hata hivyo pamoja na upatikanaji huu, wakulima na wauzaji wengi hawajafikiria namna ya kuongezea thamani zao hili ili kuzalisha bidhaa bora zaidi zenye soko na muda mrefu wa matumizi. Mkulima Mbunifi unashauri kusindika nazi na kuzalisha bidhaa hizo ili…
Ijue teknolojia ya vijidudu vidogo vidogo na matumizi yake katika kilimo
Kumekuwa na changamoto kadhaa za kwenye kilimo ikiwemo kukosekana na rutuba magonjwa na wadudu waharibifu. Teknolojia ya EM imekuwa ikitumiwa nchi mbali mbali duniani na pia Tanzania. Baadhi ya maeneo ya ardhi hayana rutuba kutokana na mambo kadhaa kama vile kulimwa kwa muda mrefu au matumizi ya mbolea za viwandani. Ingawaje mbolea za viwandani zinasaidia kuongeza rutuba, lakini ni…
Fahamu aina mbalimbali za viungo muhimu kwa afya ya binadamu
Pamoja na viungo kutumika kuongeza ladha katika vyakula, pia vina manufaa katika mwili wa binadamu. Mara nyingi wakulima wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mazao muhimu kwa manufaa ya jamii, ilhali wao wakijisahau kuwa wanahitaji pia kutumia ili kuimarisha afya zao. Viungo mbalimbali kama tangawizi, vitunguu saumu, vitunguu maji, pilipili na limao ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili. Je ni…
Utunzaji, uhifadhi na usafirishaji bora wa maziwa
Ni muhimu kujua baadhi ya mambo ambayo husababisha maziwa kuharibika ili uweze kuzuia hasara zisizokuwa za lazima. Maziwa yana virutubisho vingi sana. Kwa sababu hiyo, bakteria waharibifu huweza kukua kwa haraka kwenye maziwa. Kwa wasafirishaji wa maziwa, nii muhimu kufahamu vyema jinsi maziwa yanavyoweza kuharibika haraka kama hayatatumika na kuhifadhiwa vizuri au hayatasafirishwa kwa haraka. Ni muhimu kuwa na uelewa…






