- Binadamu

Ujue ubuyu na faida yake katika mwili wa binadamu

Sambaza chapisho hili

Ubuyuni tunda ambalo hupatikana katika miti jamii ya Adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbalimbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia ili kuongeza ladha wengine huchanganya ubuyu na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha ya ubuyu.

Ubuyu umekuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu. Ni tunda la asili na linapatikana porini hasa katika kanda kame (Semi arid). Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Faida za ubuyu

Ubuyu una uwezo mkubwa kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha mifupa , kusaidia mfumo wa umeng’enyaji chakula kupunguza maumivu, uvimbe na kusisimua utengenezaji wa seli na tishu mpya. Pia kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa sugu.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa:-

  1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
  2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kalisiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
  • Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
  1. Ina virutubisho vya kulinda mwili
  2. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni muhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
  3. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
  • Huongeza nuru ya macho
  • Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
  1. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
  2. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Juice ya ubuyu

Juisi ya ubuyu ni moja kati ya juisi zilizopata wanywaji wengi duniani kote katika miaka ya hivi karibuni, Juisi ya ubuyu ina virutubisho vya kalsiamu (Calcium) na madini ya chuma (Iron) ambavyo ni muhimu katika miili yetu hasa kwa watoto,
wajawazito na wazee.

Jinsi ya kuandaa juice ya Ubuyu

  1. Katika kuandaa juisi ya ubuyu unahitajika kuwa na ubuyu wa unga au wa mbegu, maji safi, sufuria, kijiko au mwiko, sukari, chujio, jagi na jiko.
  2. Kwa ubuyu wa unga;changanya vikombe 6 na maji vikombe 9.
  3. Kwa ubuyu wa mbegu; changanya vikombe 3 na maji vikombe 12.
  4. Weka sukari kiasi unachotaka, changanya vizuri na mwiko kisha bandika jikoni acha ichemke kwa kiasi cha kutosha ili kuuwa vijidudu vya magonjwa kama vitakuwemo na itakuwa tayari kwa matumizi.
  5. Acha ipoe, alafu koroga na uweke katika jagi tayari kwa kunywa.

Matumizi

Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

ANGALIZO: Ili upate faida za juisi ya ubuyu,  kama inavyoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

4 maoni juu ya “Ujue ubuyu na faida yake katika mwili wa binadamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *