- Mifugo

Utunzaji wa nguruwe Dume

Sambaza chapisho hili

Utunzaji wa nguruwe mara nyingi hutegemea aina ya makundi ya nguruwe na mfunmo wa ufugaji. Makundi ya nguruwe ni kama madume ya mbegu, majike wazazi, watoto, na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama au mafuta. Nguruwe wanaweza kufugwa ndani au nje ya banda, kutegemea na ukubwa wa shamba, kipato kilichopo kwa shughuli za ufugaji.

Ili kuleta mafanikio na tija katika ufugaji wa nguruwe ni vema kuzingatia utunzaji bora ikiwa ni pamoja na aina ya banda, uchaguzi wa nguruwe wazazi, ulishaji, udhibiti wa magonjwa na uangalizi kwa ujumla.

1.0 Utunzaji wa dume la Mbegu

utunzaji bora wa dume unaanza kwa kuchagua dume bora kwa ajili ya uzalishaji. Uchaguzi wa dume la kuzalisha ni muhimu kuliko uchaguzi wa jike kwa sababu dume moja hutumika kuzalisha nguruwe wengi katika kundi.

1.1 Uchaguzi wa Dume bora
Wakati wa kuchagua dume mfugaji anashauriwa kuzingatia yafuatayo:-

  • Achaguliwe kutoka kwenye koo wenye historia ya kukua haraka, kukuza watoto wengi na kuwatunza, kutokuwa na magonjwa au kilema cha kurithi.
  • Awe na miguu imara, mchangamfu na mwenye afya bora
  • Awe na umbile zuri linaloendana na aina yake na misuli imara itakayomwezesha kuoanda bila matatizo
  • Awe na kende mbili, kubwa, zilizokamilika na zinazolingana
  • Awe anayekua haraka na mwenye uwezo mkubwa wa kubadili chakula kwa matumizi ya mwili kuwa nyama
  • Awe na chuchu zisizopungua 12
  • Asiwe na mahisiano ya kinasaba (kama kaka na dada, mtoto na mama au mtoto na baba) na maike anayotegemea kuyapanda
  • Awe mrefu na mgongo ulionyooka

1.1 Ulishaji wa dume 

Dume kwa ajili ya kupandisha apewe chakula bora chenye viini lishe vya kutosha vitakavyotosheleza mahitaji ya mwili bila kumfanya mnene sana au kukonda. Wakati wa msimu wa upandishaji alishwe chakula bora kiasi cha kilo 2.7 hadi 3.6 kwa siku. Wakati ambao sio msimu wa kupandisha, dume apewe chakula bora kiasi cha kilo 2 kwa siku. Kwa matumizi mazuri ya chakula hicho kigawanywe na kulishwa mara mbili kwa siku. Pia inatakiwa dume apewe maji safi na salama ya kutosha kila siku wakati wote.

1.2 kinga dhidi ya Magonjwa na Wadudu

Uzuiaji wa magonjwa na wadudu ni muhimu kwa afya ya nguruwe dume. Mfugaji anashauriwa kumwona mtaalam wa mifugo aliyekaribu nae ili kupata ushauri juu ya chanjo muhimu ka ajili kuzuia magonjwa kwa wanyama wake. Mfano kwenye sehemu ambazo ndorobo, mfugaji anashauriwa kutumia chanjo.

Kuzuia wadudu, mfugaji anashauriwa kuogesha nguruwe kwa dawa za kuogeshea angalau mara mbili kwa wiki ili kuzuia ukurutu na matatizo mengine ya ngozi. Kuzuia minyoo mfugaji anashauriwa kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu. Ni muhimu banda, vifaa vya kulishia na kunyweshea maji viwe safi wakati wote.

1.3 Utaratibu wa kutumia Nguruwe dume kupanda

Upandishaji wa nguruwe unaweza kufanyika kwa njia mbili, ya kutumia dume au uhamilishaji. Njia ya kutumia dumendio inayotumiaka hapa nchni kwa utaratibu ufuatao:-

  • Nguruwe dume aruhusiwe kupanda kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miezi nane hadi kumi
  • Akiwa na umri wa miezi 10 hadi 18 anaruhusiwa kupanda mara moja kwa wiki
  • Akiwa na miezi 18 hadi 24 anaruhusiwa kupanda mara nne hadi tano kwa wiki
  • Dume wakubwa wasitumike kupanda majike wadogo kwani wanaweza kuleta madhara kama vile kuwavunja migongo.
  • Dume aruhusiwe kuendelea kupanda mpaka umri wa miaka 5 hadi 6.

Mfugaji anashauriwa kuwa, ni muhimu dume la kupandisha liwekwe kwenye chumba chenye eneo la mita za eneo 9.3 ili kuweza kupata mazoezi ya mwili ikiwa sehemu ya kupanda imetenganishwa eneo liwe la mita mraba saba. Madume yatenganishwe na Majike ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *