- Binadamu, Kilimo, Mimea

Ijue teknolojia ya vijidudu vidogo vidogo na matumizi yake katika kilimo

Sambaza chapisho hili

Kumekuwa na changamoto kadhaa za kwenye kilimo ikiwemo kukosekana na rutuba magonjwa na wadudu waharibifu. Teknolojia ya EM imekuwa ikitumiwa nchi mbali mbali duniani na pia Tanzania.  

Baadhi ya maeneo ya ardhi hayana rutuba kutokana na mambo kadhaa kama vile kulimwa kwa muda mrefu au matumizi ya mbolea za viwandani. Ingawaje mbolea za viwandani zinasaidia kuongeza rutuba, lakini ni ghali na sio salama kwa afya ya mimea, ardhi husika na hata kuzalisha mazao ya kilimo kwa matumizi ya binadamu.

EM.1 ni teknolojia inayotumia vijidudu vidogo vidogo ambao hawaonekani kwa macho wenye kuleta matokea chanya katika kilimo, mifugo, utunzaji mazingira na pia kuboresha mitambo ya gesi asilia.

Teknolojia ya vijidudu vidogovidogo inayofahamika kitaalamu kama Effective micro-organisms kwa jina la EM.1® inasaidia kupambana na changamoto kuu mbili za uzalishaji na kupunguza kabisa utegemezi wa mbolea za viwandani na madawa hasa kwa mkulima mdogo.

Jinsi ya kutumia EM

  • Tumia EM kwa kumwagilia kwenye shamba lako ambalo umetumia samadi kwenye udongo.
  • Weka milimita 40 kwenye maji lita 20 kila unapomwagilia au lita moja katika kila lita 500 za maji ya kumwagilia.
  • Tumia njia ya kupulizia mazao yako, miti ya matunda kwa wiki mara moja. Kwa kila lita moja (1) ya EM kwa lita 15 za maji ama bomba la kupulizia.
  • Weka EM kwenye samadi kabla ya kuitumia shambani unaziandaa ili ziwe tayari kwa urutubishaji ardhi.

Faida ya matumizi ya EM

  • EM husaidia samadi kuoza haraka na kuwa bora sana na hivyo kuondoa changamoto ya rutuba
  • Husaidia kupunguza magonjwa ya udongo na pia kuupa mmea kinga hasa kwa njia ya upuliziaji
  • Husaidia katika utengenezaji mboji na kufanya mboji iwe bora.
  • Hufanya mbegu kuota haraka
  • Husaidia kuboresha viua wadudu wanaotengenezwa kwa malighafi za kienyeji kama miti na majani yanayoua wadudu mashambani
  • Huboresha mazao kwa utamu na uwezo wa kukaa halisi kwa muda mrefu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Dr. Swai kwa simu +255 756 446 468 Dar es Salaam, +255 755 556 661 Arusha

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *