Janga la Covid-19 linachangia changamoto ya usalama wa chakula na lishe bora duniani. Kuwepo na mfumo endelevu wa chakula na mahali panapoweza kuhakikisha usambazaji wa chakula bora katika nyakati kama hizi, ni fursa ambazo miji michache ulimwenguni zinafurahia. Nchi nyingi na mashirika yanaongeza jitihada za kufanya kilimo salama, ili kupambana na changamoto za usalama wa chakula, ambao unaweza kusababisha janga…
Binadamu
Lishe bora ni muhimu kwako na kwa familia yako
Kuna uhusiano mkubwa kati ya kile tunachokula, hali ya afya yetu na uwezo wa miili yetu kupambana na magonjwa na vimelea vinavyosababisha magonjwa. Chakula bora kwa afya zetu na watu wanaotuzunguka ni muhimu kwa ajili ya kuendelea kuzalisha mali na kujenga jamii iliyo bora. Kuwa na afya njema, inatukumbusha wazalishaji wa mazao ya kilimo juu ya aina ya chakula tunachozalisha…
Ni muhimu kuwa kwenye vikundi ili kupata maendeleo thabiti
Mara nyingi nimesikia na kuona MkM Mkisisitiza wakulima na wafugaji kujiunga kwenye vikundi, je kuna umuhimu gani, na ni hatua zipi za kisheria tunazopaswa kufuata ili vikundi vyetu vitambuliwe na kuwa rasmi?-Bakari Buhari, Msomaji MkM Handeni. Kikundi ni muunganiko wa watu wenye nia/lengo moja katika kutekeleza jambo fulani walilolikusudia kwa faida ya hao walioamua kuwa pamoja. Lengo kuu la kuwa…
Je tunajali lishe bora kwa ajili ya watoto wetu kila siku
Tofauti na ilivyo kwa watu wazima, watoto wanahitaji kupata lishe bora kila siku ili kuweza kujenga miili yao, na kukua katika kiwango kinachotakiwa na hatimae kuwa watu wazima. Ni muhimu kufahamu lishe inayotakiwa kwa watoto. Lishe bora ni nini? Lishe bora ni mlo unaojumuisha uwiano unaotakiwa wa virutubisho vyote muhimu vinavyotakiwa kutoka katika makundi makubwa ya vyakula. Miili yetu huhitaji…
Madhara ya kiafya kutokana na viuatilifu
Wakulima wengi wamejisababishia madhara ya kiafya kutokana na matumizi ya viuatilifu. Hii ni kutokana na kutokua na maarifa sahihi na kutokutumia hatua zinazostahili za kinga au kutekeleza mbinu sahihi za udhibiti. Viuatilifu vya kiwandani na zana zake kwa kawaida huhifadhiwa majumbani ambako kuna hatari ya kugusana na chakula na watoto. Pia mazao yaliyopuliziwa dawa wakati mwingine huvunwa bila ya kuzingatia…
Wakulima Waliotia fora
Augustino Olturia: Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa “Nimefanya shughuli za kilimo na ufugaji toka mwaka 1984. Sikuwa nimefahamu kuwa naweza kuwalisha ng’ombe wangu kwa kipimo na nikapata mafanikio mpaka niliposoma jarida la Mkulima Mbunifu.” Ni maneno ya Mkulima msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu Bw. Agustino Olturia kutoka Kijiji cha Oloigeruno Mkoani Arusha. Bwana Agustiono anasema kuwa jarida la Mkulima…
Tumia mazao funikizi kwa chakula na kulisha mifugo
Mazao funikizi siyo mageni sana kwa wakulima walio wengi isipokuwa kwa wale ambao ndio kwanza wanaanza kujiingiza katika kilimo hifadhi. Si mazao yote funikizi yanayoweza kutumika kulishia mifugo moja kwa moja mara baada ya kuvuna kutoka shambani. Mengine ni lazima yafanyiwe maandalizi fulani ndipo yatumike kulishia. Mazao funikizi kama vile, canavalia yanahitajika kukaushwa kwanza na kuandaliwa vyema kabla ya kulisha…
Raphael: Mkulima asiyeona anayeendesha maisha yake kwa kilimo
Ukimuona akiwa shambani anavyojituma huwezi kumdhania kuwa ana ulemavu wa macho. Analima bila kupumzika, na hata katika maongezi, huongea huku akiendelea na shughuli zake kama kawaida. Kuna msemo usemao,
Fahamu ugonjwa hatari wa mahindi MLN
Fahamu ugonjwa hatari wa mahindi MLN Ugonjwa hatari wa mahindi ujulikanao kwa jina la kitaalamu








